Monday, November 7, 2016

MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA KITUO CHA HUDUMA SHIRIKISHI DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure, hii leo.

Na BMG

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizindua jengo la kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizindua jengo la kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Antony Binamungu ambaye ni mlinzi wa mtoto na ukatili wa kijinsia kutoka shirika la PACT Tanzania, akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Notigela Ngaponda, akizungumza kwenye uzinduzi wa Kituo cha Pact Tanzania
Viongozi mbalimbali
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Notigela Ngaponda, akizungumza na wanahabari ambapo amesema kituo hicho kitarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya Sekour Toure

Na George Binagi-GB Pazzo


Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka maafisa ustawi wa jamii kwa kushirikiana na askari polisi kitengo cha dawati la jinsia, kufikisha elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wananchi ili kusaidia mapambano dhidi ya vitendo hivyo.

Mongella ametoa agizo hilo wakati akifungua kituo cha huduma Shirikishi dhidi ya Ukatili wa kijinsia na watoto cha One Stop Centre kilichojengwa na taasisi ya Pact Tanzania kwa ufadhiri wa watu wa Marekani, katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekour Toure.

Amesema hatua za kukabiliana na ukatili wa kijinsia zinapaswa kuchukuliwa mapema badala ya kusubiri utokee katika jamii ambapo amesema watakaokuwa wakipatikana na hatia za kujihusisha na ukatili wa aina hiyo watachukuliwa hatua za kisheria mara moja.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sekour Toure, Dkt.Leonard Subi, amesema kituo hicho kitajumuisha watumishi mbalimbali ikiwemo polisi, maafisa ustawi wa jamii pamoja na wataalamu wa afya kwa ajili ya kuwahudumia wahanga wa vitendo vya ukatili wa kinjinsia ambavyo bado vimeshamiri mkoani Mwanza.

Amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwezi julai hadi septemba, wananchi 238 mkoani Mwanza wamepatiwa huduma za ukatili wa kijinsia katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya na kati ya hao 77 ni ukatili wa watoto. Kituo hicho tayari kimehudumia watu wazima 30 waliolengwa na ukatili wa kijinsia huku watoto wakiwa ni 67.

Naye Antony Binamungu ambaye ni mlinzi wa mtoto na ukatili wa kijinsia kutoka shirika la PACT Tanzania, amesema ujenzi wa kituo hicho umegharimu shilingi milioni 80 ikiwa ni pamoja na gharama za vifaa na mafunzo ambapo kinakuwa kituo cha nane nchini miongoni mwa vituo vya One Stop Centre.

No comments: