Sunday, November 27, 2016

MCHENGERWA:NAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KATIKA KUPINGANA NA UFISADI

Mbunge wa jimbo la Rufuji Mohamed Mchengerwa wa pili kutoka kushoto,na wa kwanza ni Mke wa Mbunge Bi. Farida Mchengerwa wakiwa na baadhi ya kinamama wakati wa uzinduzi wa Vicoba endelevu jimboni humo.

Mbunge wa jimbo la Rufuji Mohamed Mchengerwa wa katikati akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na umoja wa kinamama wa Rufuji.


Wakinana wakifurahi kwa kucheza wakati wa uzinduzi wa Vicoba Endelevu katika jimbo la Rufiji zoezi liloongozwa na Mbunge wa Jimbo Hilo Mohamed Mchengerwa hayupo pichani.

MBUNGE wa Rufiji,Mohamed Mchengerwa (CCM),amesema atapambana na  ufisadi unaofanywa na watu wasio waaminifu katika vikundi vya kuweka na kukopa vilivyopo katika jimbo hilo,kuhakikisha fedha zinazopatikana zinatumika kwa matumizi sahihi.

 Mchengerwa alisema hiyo ni njia ya kumuunga mkono rais John Magufuli ambaye anapingana na ufisadi kila kukicha na anachukia watu wajanja wajanja wanaojipatia fedha kwa njia za udanganyifu.

Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana  wakati wa uzinduzi wa vikoba endelevu ambavyo vimejumuisha vikundi tisa ambapo hadi sasa akiba Zaidi ya milioni 45.

 ‘’Pamoja na jitihada hizi za kuhakikisha tunajikwamua na umasikini kwa kujiunga katika vikundi ili tuweze kusaidiana kirahisi bado kuna watu ambao wanafanya ufisadi ili kuviua vikundi,nitakwenda kushughulika nao wote ikiwa ni njia ya kumuunga mkono rais wetu John Magufuli ambaye kila kukicha anapingana na mafisadi’’

 Mchengerwa ambaye baada ya uzinduzi wa vikoba hivyo alichangia shilingi 6,500,000 na kuahidi kutoa milioni mbili zingine aliwataka wanavikundi hivyo kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika katika maendeleo na kuonya wenye mtindo wa kugawana fedha zinapotolewa.

‘’Naomba fedha hizi zitumike katika matumizi sahihi,nakumbuka hivi karibuni nilitoa pikipiki katika vikundi lakini taarifa zilizopo ni kwamba watu wameenda kuuza na kugawana fedha jambo ambalo si sahihi,tunajirudisha nyuma wenyewe’’alisema Mchengerwa

 Alisema wananchi wa Rufiji ni masikini na wapo nyuma kimaendeleo hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anakuwa mstari wa mbele kuukataa umasikini huo kwa vitendo.

 ‘’Nimejitolea kusaidia watu wa Rufiji kwa kuwa mlinichagua ili niwawakilishe,naombeni kila mmoja aguswe na umasikini tulionao na awe na dhamira ya dhati ya kuutokomeza,vikundi hivio vitumike vizuri mkopeshane muweze kuendesha na kuanzisha biashara zenu,naahidi kuwa bega kwa bega na nyie na leo hii (juzi) nawakabidhi mke wangu Farida Mchengerwa kuwa mlezi wenu ili msaidiane’’alisema Mchengerwa

 Kwa upande wa mlezi wa vikundi hivyo,Farida Mchengerwa,aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kujiunga na vikundi hivyo ili waweze kukopesheka kwani inajulikana kuwa masikini hakopesheki kutokana na masharti yanayowekwa na taasisi za fedha ambayo wengi hawana uwezo wa kuyamudu.

 Akizungumza kwa niaba ya wanavikundi hivyo,Abdulrahman Hafidh,alisema vikundi hivyo kwa sasa vina wanachama zaidi ya 220,kutaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na uelewa mdogo wa wanavikundi kuhusu vicoba endelevu jambo ambalo Mchengerwa aliahidi kulishughulikia kwa kumuwezesha mwalimu ili aendelee kuwapa elimu.

No comments: