Familia ya Marehemu Joseph Mungai ikiwa imeshikana mkono ishara ya upendo wakati wa mazishi ya baba yao mjini Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa. |
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika mazishi ya Mzee Joseph Mungai huko Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa. |
Waziri mkuu mstaafu Mhe. Frederick Sumaye akitoa salama zake kwa niaba ya mwenyekiti wa Taifa wa Chadema katika mazishi ya Mzee Joseph Mungai huko Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa. |
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu na waombolezaji wengine wakitoa heshima za mwisho katika mazishi ya Mzee Joseph Mungai huko Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa. |
Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule akitoa heshima zake za mwisho |
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi Mhe. Wiliam Lukuvi akiteta jambo na mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu wakati wa mazishi ya marehemu Mungai. |
Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na maendeleo
ya makazi ,Wiliam Lukuvi aongoza mamia ya waombolezaji
katika mazishi ya aliyekuwa waziri wa Elimu na mbunge
wa mstaafu wa jimbo la Mufindi kaskazin Joseph Mungai.
Akizungumza katika ibada ya mazishi
jana mjini Mafinga wilaya ya Mufindi Lukuvi ambae
alimwakilisha Rais Dkt John Magufuli alisema kuwa Mungai atakumbukwa kwa uongozi wake
uliotukuka hasa katika misingi mizuri ya elimu wa Elimu ya Sekondari (MMES)
Lukuvi alisema
kuwa wakati serikali ilipoanzisha suala la Sekondari za Kata, Mafinga na
Mufindi kwa ujumla mwamko huo ulishaanza toka miaka ya 1980 ambayo kwa uongozi
wake kama Mbunge alihamasisha Wananchi kutoa michango, kufyatua
matofalina kina mama kuchota maji yote hiyo nji katika kufanikisha adhima
ya kusogeza elimu ya sekondari kwa watu wengi
“Alianza kuwa kiongozi akiwa na umri mdogo
kuliko wanasiasa wote wa Mkoa wa Iringa wakati huo, lakini pia alikuwa
kiunganishi pale kunapotokea misuguano yoyote hakuwa na makuu na kama ulikuwa
ukitaka ushauri basi utaupata kwa mzee wetu mungai ,” alisema.
Akiongoza ibada ya mazishi askofu wa KKKT dayosisi ya Iringa Dkt Owdenburg Mdegella alisema kuwa kila mwanadamu aishie chini ya
hili jua anapaswa kuishi maisha ya kumuabudu mungu na kuachana na tabia ya
kuhukumiana hapa duniani kwakuwa kila mtu atajibu dhambi zake akiwa mbinguni .
Dkt Mdegela alisema Mungai ni moja kati ya
viongozi wachache waioacha historia kubwa hapa nchini kutokana na uongozi wake
uliotukuka wa kupigania maendeleo ya watanzania bila ya ubaguzi wa Aina yoyote.
“Leo tumempoteza mtu muhimu sana ndugu
yangu Lukuvi...mimi na wewe tunapaswa kukaa chini na kuangalia
mustakabali wa mkoa wetu wa Iringa. Ameondoka mzee Peter Siyovvela ameondoka Adam Sapi na leo ameondoka
mzee wetu Mungai sasa ni wakati wetu kwani kwa Iringa tumebaki mimi na wewe
sasa tukutane kabla mwaka haujaisha ili kujadili jambo hili alisema” Mdegella
SUMAYE
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama cha
Demokrasia na maendeleo Chadema Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye
alisema kuwa Taifa la Tanzania kimepoteza kiongozi makini aliyekuwa na uthubutu
wa kutenda mambo bila ya ubaguzi na kusimamia kile anacho kiamini katika
kuwatumikia watanzania.
Alisema kuwa Mungai alikuwa ni mtu
mchapakazi aliyekuwa na hoja alizozijenga na kuzisimamia kikamilifu kwani
alitamani sana kutenda mambo kwa haki bila ya kubaguana kiitikadi bali
alisimama katika haki.
Alisema kuwa chama cha demokrasia na
maendeleo chadema kimesikitiswa sana na kifo chake kwani alikuwa ni mtu mpenda
demokrasia hivyo katika muuenzi na kutambua mchango wake Hapa nchini
watanendeleza kudumisha misingi mizuri ya demokrasia aliyokuwa akiishi marehemu
Mungai
Luhavi
Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu wa chama
cha mapinduzi Rajabu Luhavi alisema
Mungai atakumbukwa kwa uongozi wake uliotukuka kwa wa kuwatumikia watanzania
bila ya ubaguzi.
“Alikuwa kiongozi mzuri tangu uongozi wa
Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Ametoa mchango mkubwa kwenye
maendeleo ya nchi yetu. Tunapaswa kuenzi yale mazuri waliyoyafanya na sisi
tunaanzia pale alipoishia.
Akizungumza wasifu wa marehemu Denis
Mungai alisema kuwa Mungai aliwahi kuwa Mbunge wa Mufindi kupitia CCM kwa
miaka 35.
Pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali
serikalini enzi za utawala wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na
pia katika awamu za pili, tatu na nne.
Baadhi ya nyadhifa alizowahi kushika kwa
nyakati tofauti ni uwaziri wa iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni, Waziri wa
Kilimo na Maendeleo ya Mifugo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wabunge
Baadhi ya wabunge wa majimbo ya Mkoa wa
Iringa wakizungumzia Mungai huku kila mmoja akisema alikuwa kiongozi mkweli
aliyesimamia alilokuwa analiamini.
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter
Msigwa (Chadema), alisema Mungai alikuwa kiongozi wa wazi asiyegopa kusimamia
ukweli.
Alisema amepokea kwa mshtuko taarifa ya
msiba huo na kubainisha kuwa alimfahamu Mungai akiwa nje ya ulingo
wa siasa.
“Alikuwa kiongozi mzuri tangu uongozi wa
Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Ametoa mchango mkubwa kwenye
maendeleo ya nchi yetu, tunapaswa kuenzi yale mazuri waliyoyafanya na sisi
tunaanzia pale alipoishia.
“Alikuwa kiongozi muwazi na alituunga
mkono wapinzani ingawa hakushinda… kwa ujumla alikuwa mtu mkweli asiyefungamana
na siasa za upande wowote,” alisema Msigwa.
Mbunge wa Mafinga mjini Cosato Chumi
alisema kuwa watu wa Mafinga na Mufindi kwa ujumla wamempoteza mtu
muhimu sana kwani atakumbukwa kwa mengi aliyofanya hasa mwamko na
kuisogeza elimu ya sekondari kwa watu wa kawaida kupitia Mufindi Education
Trust-MET.
Chumi alisema kuwa wakati serikali
ilipoanzisha suala la Sekondari za Kata, Mafinga na Mufindi kwa ujumla mwamko
huo ulishaanza toka miaka ya 1980 ambayo kwa uongozi wake kama Mbunge
alihamasisha Wananchi kutoa michango, kufyatua matofali na kina mama
kuchota maji katika kufanikisha azma ya kusogeza elimu ya sekondari
kwa watu wengi.“Kwa jitihada zake mzee Mungai Mufindi
ndio Wilaya ya Kwanza hapa nchini kuwa na Bank ya Wananchi yaani Community Bank
(Mucoba) ambayo imeendelea kuwa kimbilio la tabaka la chini na Kati katika
suala zima la mikopo na huduma za kibenki.
"Mimi nawaombea faraja
wanafamilia wote katika kipindi hiki cha majonzi. Mungu ailaze Roho yake Mahali
Pema Peponi - Amina alisema Chumi ”.
No comments:
Post a Comment