Kwa mtazamo mwingine wakuelimishana na maadili ya sanaa za Karate toka katika chimbuko lake huko visiwani Okinawa na hatimae jinsi mambo yanavyo badilika hadi bara ya Japan. Leo tunapenda tu kukumbushana maadili na utamaduni tofauti kwa wana Karate na kunufaishana jinsi ngazi zinapopanda juu na historia yake inazidi kupanda kielimu ya sanaa.
Mpaka utakapotembelea katika visiwa vya chimbuko la Karate, Okinawa, ndipo utakapokuta ukweli wa mambo mengi usiyofahamu kuhusiana na Karate asilia ya Okinawa.
- Stances : Okinawa zao zipo juu kulinganisha na Japan bara sababu kubwa ni kuwa ”Natural stances”. Okinawa haisisitizi “Deep staces.
- “Imi” neon linamaana msisitizo wa “Kwa nini” unafanya hiyo mbinu kuirudia techniques tena na tena. Wakati Japan Karate inasisitiza jinsi gani mbinu ifanywe kulikoni kwanini unaifanya hiyo mbinu. Okinawa Karate inatumia “Bunkai” uchambuzi wa maana ya utumiaji mbinu.
- Neno “Oss/Osu” hili neon halitumiki kabisa visiwani Okinawa, lakini limesambaa hasa nchi za magharibi na maarufu sana katika utumiaji kwenye sanaa za Brazilian Jiu-Jitsu na MMA pia. Hivyo hili neno hutolisikia kabisa likitumika katika visiwa vya Okinawa. Okinawa wanatumia neno “Hai”.
Kuna tetesi kwamba hili neon OSS/ OSU chimbuko lake ni katika vyuo vya jeshi la maji “Japanese Navy Academy”. Haikuwa na mizizi yeyote toka ilipozaliwa Karate huko Okinawa. Hivyo basi, inasemekana neno hilo lilikuzwa sana na mtindo wa Kyokushin Kai Karate ambayo mwanzilishiake ni Master Masutatsu Oyama, mzaliwa wa Korea na alikuja Okinawa kama mtoto chini ya umri wa miaka 10 na wazazi wake, hatimaye kubadili na jina kuitwa jina la Kijapan.
Katika lugha ya “Kanji” “Osu” ina maana “sukuma” na “Shinobu” maumivu, hapo ndipo neno “Osu” kama kifupi cha kuyashinda maumivu mazoezini, ukawa unatumika kuonyesha “moyoi juu!"
Hata hivyo, Okinawa Karate haijihusishi na neno “OSS/OSU kabisa, na badala yake inatumia neno “Hai” ikimaanisha kukili au kujibu kwa upole kukiri utachoelezwa mazoezini au kujibu kwa staha swali.
- Sio mchezo (Sports) ni Mwenendo wa maisha (Life style)
Mara tu baada ya kutambulishwa Japan ya bara, Karate ikaanza kutumika kimashindano na kuanza badilisha Kata nyingi ili ziweze kuendana na michezo ya mashindao huko Japan. Pia mmoja ya waasisi wa mashindano ya Kumite alikuwa Gogen Yamaguchi wa Internationa Goju Kai, waliongeza vionjo ili kuwa na pointi katika mashindano ya Sports Karate. Hata hivyo, Okinawa sasa nayo wana Sports Karate, lakini mbali sana na mlingano wa ile ya Japan bara.Watu wa Okinawa wanajivunia sana sanaa yao ya Karate kama mwenendo wa maisha na sio michezo tu.
5.Chinkuchi na Kime.
Japan ya bara, neno “Kime” au “Kimeru” ina maana ya uamuzi au “Fix” na kwa upande mwingine, Okinawa wanatumia neno Chinkuchi, ikimaanishi “ Full-body power”.
- KOBUDO
- Japanese Karate haisisitizi utumiaji wa zana za kujilinda zaidi ya mikono mitupu. Lakini huko Okinawa kila Dojo wanafundisha pia mbinu za utumiaji silaha zao asilia za Karate “Kobudo”. Hii ikinaanisha kuenzi uvumbuzi wa vifaa vyao asilia walizokuwa wakitumia kujilinda wakati wa mapambano .
- Silaha hizo ni:
Bo; Sai; Tonfa; Nunchaku; Kama; Timbe/ Rochin; Tekko; Kuwa; Sansetsu Kon; na Nunti bo. Okinawa wanaamini kwambaKarate na Kobudo na kama kaka na dada kimafunzo.
- Shule za zamani:
- Ziliendeleza vifaa vya mazoezi ya mwili kama vile Makiwara, Chishi, Ishi Sashi, Nigiri- game, Tou kwa ajiri ya kuimarisha nguvu ya mwili kimazoezi. Lakini, Japan bara utakuta Makiwara tu na sio vifaa hivyo vingine kama Okinawa.
- Tuidi Techniques.
Jinsi Okinawa inavyo sisitiza mbinu ya mapambano karibu “ Close range combat”, wakati Japan bara wanasisitiza “ Long distance range combat”..
Okinawa hutumia sana mbinu za kuvuta, pinda kibano na hata kuvunja viungo vya mpinzani wako, ambavyo havina msisitizo sana Japan ya bara. Hivyo, ukiwa Okinawa neno “Tuidi” au maarufu “Kakie” ni mtililiko wa mbinu za mikono, au kama magharibi wanaita “Pushing hands”.
Tofauti ya Ufundishaji:
Okinawa wanapendelea sana ufundishaji wa mtu mmoja mmoja kimafunzo kulinganisha na Japan bara ambao ni ufundishaji wa makundi. Dojo za Okinawa ni ndogo sana kwa sababu ufundishaji wao wa muda tofauti vikundi vidogo. Wakati Japan bara hufundisha watu 50 kwa mara moja na hii ndio tofauti katika ufundishaji wao.
- Uchinaa-guchi:Okinawa ina lugha yake tofauti “Uchinaa-guchi” Mdomo wa Okinawa!Hii imetolewa katika daftari ya makumbusho ya Karate, Mjini Naha , Okinawa na Sensei Rumadha Fundi, Sandan “Shibu-cho Tanzania” Jundokan So Honbu.
Sensei Rumadha Fundi, kulia akifanya marekebisho ya kinga na masenpai Abdul-Waheed kushoto na Yusuf Kimvuli kati, hivi karibuni katika viwanja vya basketball vya Gymkhana jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment