Monday, November 7, 2016

ARUSHA WAZINDUA SIKU YA USALAMA BARABARANI ,TWAKIMU ZAONYESHA KILA MWAKA AJALI ZA PIKIPIKI ZINAONGEZEKA

Habari Picha na Woinde Shizza,Arusha
Ajali za pikipiki kwa mkoa wa Arusha zimeongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 zilifika ajali 836 huku upande ajali za magari zikipungua kwa asilimia 11.
Hata hivyo ajali hizo za pikipiki kwa mwaka 2010 zilikuwa 709 ukilinganisha na ajali 277 za pikipiki mwaka 2009 ajali hizo za pikipiki bado zinaendelea kuongezeka.
Hayo yamebainishwa na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Selemani wakati akielezea hali ya usalama wa barabarani kwenye uzinduzi wa maazimisho ya wiki ya usalama barabarani  mapema leo.
Selemani alisema kuwa takwimu zinaonesha mkoa wa Arusha bado unakabiliwa na ajali za barabarani ambapo kwa kipindi cha mwaka 2007 ajali zimekuwa zikiongezeka na kulikuwa na ajali 1807na kufikiakiwango cha juu mwaka 2010 ambapo ajali 2658 huku kwa kipindi cha mwaka 2012 ajali zilianza kupungua hadi kufikia ajali 2011
Alifafanua kuwa baada ya jeshi kutumia nguvu kubwa sana katika kupunguza ajali zinazotokana na magari zilipungua sana ingawaje kwa sasa bado wimbi kubwa la ajali linatokana na ajali za pikipiki.
Katika hatua nyingine alisema kuwa ajali zinasababishwa na sababu za kibinadamu kwa asilimia 75,madereva kulewa huku wakiwa wanaendesha vyombo vya moto,pia ubovu wa vyombo vya usafiri kwa asilimia 15,miundombinu ya barabara kwa asilimia10.
Awali mgeni rasmi katika uzinduzi huo mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro alisema jukumu la usalama wa barabarani sio la polisi wenyewe wala kamati ya kikosi cha usalama barabarani pekee bali ni ulinzi wa kila mtu.
Fabian alisema kuwa endapo kama kila mtu atafuata sheria na kanuni za barabarani basi ajali zitakuwepo kwa kiwango cha asilimia 0.0 kwani ajali zinachangia kudidimiza mlengo wa taifa.
Hataivyo katika uzinduzi huo baadhi ya askari wa usalama barabarani walifanikiwa kupewa vyeti vya ufanyakazi bora ambapo mmoja wa askari hao Silas Konga alisema kuwa maadili yao bora kazini yamechangia wao kutambulika na jeshi hilo.
  Askari wa usalama barabarani koplo Atilio Choga akiwa anatoa maelezo mafupi ya barabara zilizopo mkoani Arusha na jinsi magari yanavyoingia na kutoka  katika siku ya uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani ilianza Jana katika viwanja vya sheikh Amri Abeid ,mbele ni mkuu wa wawilaya ya Arusha Fabian Daqarro ambapo alikuwa mgeni rasmi
 askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani akimuonyesha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Arusha jinsi kifaa chakupimia ulevi kwa madereva kinavyo fanya kazi





 kabla ya sherehe kuanza kulikuwa na maaandamano  apa askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwasili katika viwanja vya sheikh Amri Abeid kwa maandamano
 kikundi cha walemavu wao pia walijitokeza katika sherehe hizi za uzinduzi wa siku ya usalama barabarani 
 kikundi cha ngoma cha wanafunzi   nacho kilikuwepo katika sherehe hizi za siku ya usalama barabarani

 wageni waalikwa wakiwa wanafatilia uzinduzi huo leo katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid
 kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Selemani  akiwa anasoma risala
mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro katikati akiwa anaandika baadhi ya changamoto alizotajiwa 


No comments: