Thursday, October 13, 2016

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA KIWANDA CHA MAZIWA MEATU SIMIYU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kabla ya kuzindua kiwanda cha kusindika maziwa wilayani Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akiweka jiwe la uzinduzi katika kiwanda cha kusindika Maziwa wilaya ya Meatu, Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akipewa maelezo na vijana wa kikundi cha Meatu Milk wanaojishughulisha na usindikaji wa maziwa kabla ya kuweka jiwe la uzinduzi katika kiwanda cha kusindika Maziwa Meatu.
: Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akizungumza na Vijana na wananchi wa Meatu baada ya  Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  kufungua kiwanda cha maziwa Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Vijana na wananchi wa Meatu wakati wa ufunguzi wa  kiwanda cha maziwa Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi zawadi ya maziwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua kiwanda cha maziwa Meatu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mhe. Pius Machungwa akipokea zawadi ya  maziwa kutoka kwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kufungua kiwanda cha maziwa Meatu.
Baadhi ya viongozi wa Wilaya Meatu, mkoa wa Simiyu na viongozi wa kitaifa wakicheza muziki ishara ya kufurahia uzinduzi wa Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (waliokaa) wa nne) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu, na Vijana wa Meatu Milk.

Na Stella Kalinga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amefungua kiwanda cha kusindika maziwa kinachoendeshwa na  kikundi cha Vijana wa Meatu kilichopo wilayani humo Mkoa wa Simiyu.

Akizungumza na Vijana hao wanaosindika maziwa ya Meatu (MEATU MILK), Waziri Mhagama amewataka kuutunza mradi huo ili uwe mradi mkubwa wa kuwaingizia mapato wao na Serikali kwa ujumla. 

Mhagama amesema kwa kadri mradi huo utakavyokuwa mkubwa ndivyo wafugaji wa Wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla watakavyonufaika kwa kupata soko la uhakika la maziwa.

Aidha, Waziri huyo amewataka Viongozi wote wa wilaya kuunga mkono juhudi zilizofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka za kuwatengenezea  vijana mazingira mazuri ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo yao, ikiwa ni pamoja na kushughulikia upatikanaji wa mitaji na mafunzo ya kuwajengea uwezo.

Wakati huo huo Waziri Mhagama ameahidi  kuwa Ofisi yake itatoa mkopo wa shilingi 30,000,000 kwa lengo la kuwasaidia vijana hao kuongeza uzalishaji ili kupanua soko la maziwa yao ndani na nje ya Mkoa.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa Ofisi ya Waziri Mkuu itawapa mkopo vijana wa “Meatu Milk”ili wapanue uzalishaji; Wizara yangu itatoa mikopo kwa vijana walio tayari kutekeleza ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowasaidia kuwapa ajira na kujikwamua kwenye umaskini” alisema Mhagama.

Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Meatu kabla ya kumkaribisha Waziri Mhagama Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa huo umejipanga kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini.

“Tumejichagua kuwa pacha wa Mhe. Rais katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Vitendo na tumedhamiria kuwa miongoni mwa mikoa mitano inayofanya vizuri katika uchumi”, alisema Mtaka.

Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu  kwa Mhe. Waziri, kiongozi wa kikundi cha Meatu Milk Lightness Benedicto amesema Halmashauri imewapa mtaji na kuwajengea uwezo kwenye teknolojia za usindikaji, ufungishaji wa bidhaa za maziwa pamoja na elimu ya ujasiriamali.


Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Mbuzi ameahidi kuwaongezea mtaji wa shilingi 5,000,000 vijana hao pamoja na kuwasaidia kukutafuta soko la uhakika kwa maziwa watakayosindika.



No comments: