“Tukiwa tunasherehekea wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka
2016,tunajivunia kuwa sehemu ya maendeleo na mafanikio yako ya Familia
yako,tunaahidi kukupatia suluhisho la masuala ya kibenki ambayo si tu kuongeza
kasi ya ukuaji wa biashara zako, lakini pia kukuhamasisha wewe kufanikiwa
zaidi,”ilisema taarifa hiyo.
CRDB iliwashukuru wateja kwa kuichagua Benki ya CRDB
na kwamba matumaini yao ni kuendelea kufurahia huduma zao ambazo ni
za kibunifu.
“Kwa unyenyekevu na furaha kubwa,kwa niaba ya familia
ya Benki ya CRDB nachukua fursa hii kukushukuru kwa kuendelea kutumia huduma
zetu, sisi kama Benki tunaamini kwa kiasi kikubwa katika kujenga mahusiano ya
kudumu na wateja wetu, siku zote tutaendelea kushirikiana nawe katika kutimiza
malengo yako na kufurahia mafanikio tunayopata kwa pamoja".
Meneja
wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo akizungumza
na Wateja pamoja na Wafanyakazi wa Benki hiyo ikiwa ni muendelezo wa
Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba 3 Duniani kote ambapo wateja
wa CRDB wataendelea kujivunia mafanikio ya Benki hiyo.
Ofisa
Mauzo wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Mohamed Madengelo
akizungumza na wateja wa Benki hiyo katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa
Wateja.
Sherehe hiyo ilipambwa kwa keki.
Meneja
wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo
akishirikiana na mmiliki wa Kampuni ya Easy Connections, Justus Bashara
wakati wa hafla hiyo.Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina
Kinabo akisaidiana kuandaa vipande vya keki kwa ajili ya wateja na Meneja Mikopo
wa benki hiyo, Erick Mgonja.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo
akimlisha keki mteja wa Benki hiyo, Richard Mlay.
Mmiliki wa Kampuni ya HR Auto Parts Trading, Kisangeta Mihonye akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa
Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementina Kinabo.
Wateja wakiwa katika hafla hiyo.
Mmiliki wa Kampuni ya JECEN Building Contractor, Nicholous Mwalituke akitoa shukrani kwa niaba ya wateja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Justus Bashara akishukuru kwa niaba ya Wateja wenzake.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment