Tuesday, October 25, 2016
Wadau waishauri Taasisi ya Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) kuandaa upya mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa Wasanii.
Rais wa Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) Bw. Carolous Bujimu (kushoto) akielezea mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii wakati wa kikao na wadau wa tasnia ya Filamu na Muziki leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (katikati) akizungumza na wadau walioshiriki katika kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) Bw. Carolous Bujimu.
Mjumbe kutoka COSOTA Bw. Paul Makula akichangia mada wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba
Afisa Kodi Mkuu kutoka TRA Bw. Sydney Mkamba (kushoto) akizungumza na wadau wa filamu na muziki wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mrakibu Msaidi wa Polisi (ASP) Bw. Mboka Minga
Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Joyce Hagu
Mrakibu Msaidi wa Polisi (ASP) Bw. Mboka Minga (aliyesimama) akichangia wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Ubunifu kutoka Wanene Studio Bw. Rodgers Charles
…………………………………………………………
Na: Genofeva Matemu – WHUSM,
Wadau wa Tasnia ya Filamu na Muziki wameishauri Taasisi ya Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) kuandaa upya mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa kuwa na takwimu kutoka kwa Taasisi zote zinasimamia sekta ya Filamu na Muziki nchini.
Rai hiyo imetolewa na wadau mbalimbali wa tasnia hizo walioshiriki katika kikao kilichoandaliwa kwa ajili ya kuwasilisha mwongozo huo kwa wadau leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba amesema kuwa ni vyema mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kutoka TCDB kuzingatia takwimu na taarifa sahihi kutoka kwa wadau ili kuweza kuendana na hali halisi ya tasnia hizo.
“Katika kutekeleza azma ya Taasisi ya TCDB ni vyema mkaandaa mchakato wa kufikia na kushirikisha vyombo vya wadau kuanziia ngazi ya chini kwa kupitia shirikisho la filamu pamoja na Taasisi za Serikali ambao watachangia katika kuandaa mwongozo ulio bora” amesema Bw. Mwakifwamba.
Aidha Mrakibu Msaidi wa Polisi (ASP) Bw. Mboka Minga ameitaka Taasisi ya TCDB kuandaa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji ili uweze kuendana na jitihada zilizofanywa na Serikali katika kusimamia na kupambana na maharamia wa kazi za sanaa.
Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo ameitaka Taasisi ya TCDB kushirikisha wataalamu wa tasnia ya Filamu na Muziki ili waweze kuendesha Taasisi hiyo kitaalamu na kwa weledi.
Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) ni Taasisi ambayo inalenga kusimamia na kukuza vipaji vya wasanii wa filamu na muziki kuanzia ngazi ya Wilaya kwa kuibua na kusimamia uandaaji wa kazi za sanaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment