TABIA ya vijana kutojishughulisha katika miradi mbalimbali yenye tija kumeeelezwa kuwa moja ya vyanzo vya kudorora kwa uchumi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Mh. Jenista Mhagama katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la vijana
lililofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Allience Mjini Bariadi.
Alisema kumeanza kujitokeza hali
ambapo vijana nchini kutokupenda kujishughulisha katika miradi
mbalimbali ya kiuchumi na hivyo kushindwa kuondokana na umaskini na pia
kuchangia katika pato la taifa.
Alisema kuwa vijana wanaongoza
kwa idadi kubwa lakini wanashindwa kujishughulisha kuhakikisha wanapata
maendeleo ambayo yanaweza kulisaidia taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida (kushoto)
akisalimiana na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge,
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama (kulia)
alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi
kufungua kongamano la vijana.
Mhagama alisema katika Kongamano
hilo ambalo limeandaliwa na Mkoa wa Simiyu, kuratibiwa na Taasisi ya
utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwamba kuna fursa nyingi lakini
vijana wanakuwa wagumu kuzichangamkia na matokeo yake kubaki
wakiilalamika serikali kuwa haiwajali.
Alibainisha kuwa serikali itaendelea kusaidia makundi ya vijana yanaoonesha nia ya kujiendeleza
Aidha alifafanua kuwa
itawaongezea mtaji wa shilingi milioni 30 kwa kikundi cha vijana
cwalioanzisha kiwanda Maziwa cha Meatu pamoja na kile cha Chaki kutokana
na jitihada zao walizofanya na matunda kuonekana.
Awali kabla ya kumkaribisha mgeni
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema lengo la serikali mkoani
hapa ni kuhakikisha linainua pato la mkoa na kuchangia katika pato la
taifa kwa kuwawezesha vijana wake kutengeneza bidhaa zinazotokana na
malighafi zinazozalishwa mkoani hapa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista
Mhagama na Naibu wake Mh. Anthony Mavunde wakisalimiana na baadhi ya
viongozi wa mkoa wa Simiyu na ESRF mara baada ya kuwasili kwenye
kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana katika ukumbi wa shule
ya msingi Allience mjini Bariadi.
Alisema zaidi kwamba wanalengo la kuhakikisha mkoa unaingia katika tano bora ya uchangiaji wa pato la taifa.Amehimiza viongozi kuwasaidia vijana kuwaongoza, kuwaelekeza na amewataka vijana kuwa na uthubutu na kuungana kwa pamoja.Pamoja na harakati za kiuchumi
vijana wametakiwa kuwa na mwendo wenye maadili mema ili kuendelea kuwa
na afya bora na kukwepa magonjwa yanatokanayo na ukosefu wa maadili.Amesistiza kuwa kauli mbiu
waliyoanzisha ya “Bidhaa moja,wilaya moja” itumike ipasavyo ili
kufanikisha maendeleo yao na ya wilaya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista
Mhagama akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la vijana Simiyu
lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini
Bariadi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida alisema
ushiriki wa vijana katika viwanda vidogovidogo kunaweza kukuza uchumi
kutokana na viwanda hivyo kutoa ajira na pia kutengeneza mnyororo wa
thamani katika mazao ya wakulima ambako vijana ndiko wanakotarajiwa
kuonesha ushujaa wao.
Hata hivyo alisema ukuaji wa
uchumi kwa sasa bado ni changamoto kwa wananchi wanaoishi vijijini
kutokana na baadhi ya huduma kutowafikia kwani asilimia 7 inayopanda
kiuchumi huwa haitafsiriki kufikia makundi yote ya kijamii .
“Tumekuwa tukiendesha tafiti
nyingi lakini tunaona kipato chetu kinaendelea kushuka hasa katika
wananchi wanaoishi vijijini hivyo kuwepo kwa viwanda kutaweza kuwainua
kiuchumi wananchi kutokana na bidhaa zao ghafi kuuzwa katika
viwanda”Alisema Dk. Kida.Nao wafadhili wa Kongamano hilo UNDP wamesema wametenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia vijana katika programu zao za maendeleo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Waziri Mhagama.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony
Mtaka akizungumza machache awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama kufungua kongamano la kitaifa la
vijana lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience
mjini Bariadi.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji,
Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.
Moudline Castico akitoa salamu kwa vijana kutoka visiwani Zanzibari
kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa
shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Meza kuu mgeni rasmi Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Mh. Jenista Mhagama, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee,
Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline
Castico (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk.Titus
Kamani ( wa pili kulia), Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF,
Dk. Tausi Kida (kushoto), Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Anthony Mavunde
(wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa
tatu kushoto).
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
kuondoa Umaskini wa Wizara ya Fedha na Mpiango, Mudith Cheyo (kulia) na
Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango,
Maduka Kessy wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa kongamano la
vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi
Allience mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk.
Tausi Kida akiwasilisha mada ya mageuzi ya kiuchumi yanayohitajika
kuboresha maisha ya vijana pamoja na hali ya uchumi nchini kwa makundi
ya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini walioshiriki kongamano la
vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi
Allience mjini Bariadi.
Bw. Abdallah Hassan (kushoto) na
John Kajiba wa ESRF wakifuatilia jambo kwenye kongamano la vijana
Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience
mjini Bariadi.
Mkuu wa Programu, Shirika la
Maendeleo UNDP, Amon Manyama akizungumzia mchango wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa (UN/UNDP) katika Maendeleo Endelevu ya Vijana wakati wa
kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya
msingi Allience mjini Bariadi.
Sehemu ya umati wa vijana na
wageni waalikwa waliohudhuria kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika
jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Naibu Katibu Mtendaji Tume ya
Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Kessy akiwasilisha mada ya
fursa za vijana katika uchumi wa viwanda pamoja na Mpango wa pili wa
Maendeleo wa miaka mitano 2016/17-2020/21 kwenye kongamano la vijana
Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience
mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi
Stadi-VETA Leah Dotto akiwasilisha mada iliyozungumzia mchango wa elimu
ya ufundi stadi katika kufikia Tanzania ya viwanda katika kongamano la
vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi
Allience mjini Bariadi.
Afisa Mwandamizi wa Idara ya
Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Abdallah Hassan akizungumzia fursa mpya ya
kilimo biashara kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana
katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Pichani juu na chini washiriki
wakiuliza maswali kwa wakufunzi na viongozi wa serikali katika kongamano
la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi
Allience mjini Bariadi.
Pichani juu na chini ni umati wa
makundi ya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Vyuo Vikuu
waliohudhuria kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika
ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.
Jenista Mhagama na Naibu wake, Mh. Anthony Mavunde katika picha ya
pamoja na mdhamini mkuu wa kongamano hilo UNDP, waratibu ESRF pamoja na
wawasilishaji mada kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana
katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.
Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka katika picha ya
pamoja na wawasilishaji mada, ESRF pamoja na UNDP kwenye mabango ya
viwanda vilivyoanzishwa na vijana cha Meatu Milk na kiwanda cha kwanza
Tanzania cha kutengeneza Chaki cha mkoani Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony
Mtaka, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Anthony Mavunde wakimtunza
mwanakikundi wa ngoma za asili cha Wanaisanga kutoka Maswa mwenye uzoefu
wa kucheza na Chatu wakati wa burudani kwenye kongamano la vijana
Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience
mjini Bariadi.
Mwanakikundi wa ngoma za asili
Wanaisanga kutoka Maswa mwenye uzoefu wa kucheza na Chatu akionyesha
umahiri wake wa kucheza na chatu kwenye kongamano la vijana Simiyu
lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini
Bariadi.
Kutoka kulia ni Naibu Katibu
Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Kessy, Mkuu
wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon
Manyama, Mtafiti Mshiriki ESRF, Dr. Oswald Mashindano, Mkurugenzi
Mtendaji wa ESRF, Dr. Tausi Kida, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu
ESRF, Margareth Nzuki wakifurahi burudani ya ngoma za asili ya kucheza
na Chatu wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika
ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Wageni waalikwa wakiendelea kufurahi burudani ya ngoma za asili kwenye kongamano la vijana Simiyu.
Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kongamano la vijana Simiyu waliwakilisha.
No comments:
Post a Comment