MFUKO wa Uwekezaji wa Pamoja (UTT-AMIS) umesema kutokana na utafiti walioufanya kwa muda wa miaka 10, unaonyesha Watanzania walio wengi hawana uelewa wa kuwekeza fedha zao kwenye hati fungani (bond).
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT, Daudi Mmbaga , alisema watu wengi wanakuwa na fedha nyingi lakini hawajui jinsi ya kuwekeza fedha zao.
Alisema kutokana na changamoto iliyopo kwa Watanzania ya kutokuwa na uelewa wa jinsi ya kuwekeza , wameamua kuanzisha huduma ya Usimamizi wa Mali itakayomsaidia mwananchi jinsi ya kuweza kuwekeza fedha zake na kutengeneza faida.
“ Watu wengi wanakuwa na fedha nyingi lakini zimelala tu, na wengine wamewekeza kwenye maeneo yasiyowapa faida ndio maana tuamua kuanzisha huduma itakayowasaidia kuwekeza fedha yao inayoitwa Usimamizi wa Mali,” alisema.
Aidha, alisema huduma hiyo kwa sasa imeshaanza kutumika na mwelekeo ni mzuri kutokana na watu wengi kupenda kuwekeza fedha zao, ambapo kiwango cha kuanzia ni sh. Milioni tano.
Mmbaga alisema kiwango cha elimu nchini kikijikita vizuri kitasababisha kuwepo na soko la uhakika na kusababisha kuwepo na maendeleo ya kiuchumi.
Hata hivyo aliwashauri wananchi kujitahidi kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji kwa kuwa kutasaidia kuwa na imani na fedha zao.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Uwezeshaji (UTT-AMIS), Daud Mbaga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
kuhusu huduma yao mpya ya usimamizi wa mali. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji,
Issa Wahichinenda.
No comments:
Post a Comment