Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo ( wa nne kutoka kulia) katika picha ya pamoja
na wawakilishi kutoka Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB), Ubalozi wa Sweden na Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP).
Tanzania
inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano litakalokutanisha nchi
mbalimbali za Afrika kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu
katika masuala ya Nishati linalotarajiwa kufanyika Aprili mwaka 2017.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
alipofanya kikao na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini,
Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB), Ubalozi wa Sweden na Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP).
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao kilichokutanisha
wawakilishi kutoka kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB), Ubalozi wa Sweden na Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Nishati na Madini
anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe.
Wawakilishi kutoka
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Ubalozi wa Sweden na Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Wawakilishi kutoka
Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya
Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) wakifuatilia maelezo
yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi Mkazi wa na Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mkazi wa
na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo
akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Mkurugenzi Mkazi
wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi
ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo.
No comments:
Post a Comment