Saturday, October 22, 2016

TANESCO YASEMA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KUPITA ARDHINI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

 Kaimu Meneja Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ardhini, (Underground Transmission Lines), kwenye shule ya sekondaru ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2016.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

SHIRIKA la umeme nchini (TANESCO), limekamilisha ujenzi wa  mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) ,  kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo kipya cha kupozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV.

Akizungumzia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa  mfumo huo ambao utahusisha ujenzi wa mfumo wa njia za usambazaji umeme chini ya ardhi (Underground Distribution Lines), wa kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City Centre na vituo vingine vitatu vya Kariakoo, Railway na Sokoine.

Akifafanua zaidi, Mhandisi Rashidi alisema, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmision Lines),  kwa msongo wa Kv132 kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre tayari umekamilika na ule wa kutoka shule ya sekondari ya wasichana Jangwani kwenye City Centre pia umekamilika.

“Faida kubwa ambayo wakazi wa jiji la Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme wa uhakika (reliable power supply ulio kwenye viwango stahiki, (Acceptable quality power supply) hususan kwa wale wa maeneo ya katikati ya jiji,” Aliongeza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali.Akieleza zaidi, Mhandisi Nangai alisema, “Mradi huu unaviwezesha viituo tajwa kuwa na njia mbili za kuvvipatia umeme na hivyo kuwezesha kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia moja kati ya hizo itakuwa na hitilafu.” Alifafanua.

Alisema kuongezeka kwa kituo cha City Centre cha 100MVA, kunafanya jiji la Dar es Salaam pekee kuwa na jumla ya vituo 9 vya aina hiyo.
“Hivi sasa tunaweza kusema, ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98, kinachoendelea ni kukamilisha ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme kupitia juu (Overhead Transmission Lines), wa kilomita 1.3 wa msongo wa kilovolti 132 kutoka kituo kikubwa cha kupozea umeme cha Ilala hadi shule ya sekondari ya wasichana Jangwani ambapo utaungana na mfumo wa usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) kwenda kituo kikubwa cha City Centre.” Alifafanua.

kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre, umekamilikakatikati yan jiji utekelezaji wa Mradi huo, unaofadhiliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Finland, unahusisha ujenzi wa kituo cha udhibiti mifumo ya usambazaji umeme (Distribution SCADA System), katika msongo wa kilovolti 33 na 11.

“Tayari ujenzi wa kituo cha City Centre umekamilika kwa asilimia 100 na sasa tuko katika hatua za majaribio.” Alisema Mhandisi Rashidi.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, amewaomba wakazi wa jiji kuwa wavumilivu wakati zoezi hili la kuboresha miundombinu likiendelea kwani huwa panatokea kukatika kwa umeme sehemu Fulani Fulani ili kutoa nafasi kwa mafundi kufanya kazi kwa usalama zaidi.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashidi wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala,  Mhandisi Athanasius Nangali, (katikati), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashid, (kulia), Afisa Habari na Mawasiliano wa TANESCO, Hendry Kilasila, wakitembelea eneo la ujenzi wa Mfumo huo shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam
 Nguzo ya kusafirisha umeme wa juu kutoka Kituo cha Ilala kuja shule ya sekondari ya wasichana Jangwani, ambapo zitaungana na Mfuko wa njia ya kusafirisha umeme ardhini kupelekea katikati ya jiji

 Mafundi wakiwa kazini

 Mhandisi  Nangali, (mbele), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Rashid, (kulia), wakiangalia moja ya roller lenye nyaya.

No comments: