Friday, October 14, 2016

TAASISI YA LECRI CONSULT YAENDESHA WARSHA KWA VIJANA YAWATAKA WASITEGEMEE KUAJIRIWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Legal and Child Right Consult, Edna Kamaleki (kushoto), akizungumza na vijana wasomi katika warsha ya siku moja ya kuwaongezea uwezo iliyofanyika Dar es Salaam leo. Warsha hiyo iliandaliwa na taasisi hiyo.
Mdau Julius Kionambali (kushoto), akizungumza katika warsha hiyo.
Miriam Mnada (kulia), akichangia mada
Vijana wasomi wakiwa kwenye warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Vijana wakisikiliza mada kwa makini



Na Dotto Mwaibale


VIJANA wasomi wametakiwa kuacha kutegemea kazi za kuajiriwa badala yake wawe wabunifu katika masuala mbalimbali kulingana na elimu yao ili kujikomboa kiuchumi.

Mwito huo umetoewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Edna Kamaleki Dar es Salaam leo katika warsha ya siku mbili ya kuwaongezea uwezo vijana iliyoandaliwa na taasisi hiyo. 

"Kijana umesoma kwanini upoteze muda wako kwa kuzunguka kutafuta kazi wakati fursa nyingi zipo" alisema Kamaleki.Kamaleki aliwataka vijana waoshiriki warsha hiyo kubadili na kuthubutu kuanza kufanya kitu chochote kulingana na elimu walizosomea vijana hao.

Akizungumzia taasisi yake hiyo alisema imejikita kutoa huduma za kisheria kwa jamii na ushauri katika mambo mbalimbali yanayohusu haki za watoto."Tuna amani kwamba haki za watoto ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa watoto, pia watoto wanapaswa kuishi katika jamii ambayo haki za binadamu na sheria zinaeleweka vizuri na kuheshimiwa na kila raia" alisema Kamaleki.

Alisema taasisi hiyo inatoa ushauri na huduma ya kisheria kwa jamii wakiwemo watoto, watu binafsi na taasisi mbalimbali na kuandaa nyaraka mbalimbali za kisheria na mikataba ya kisheria.

Aliongeza kuwa shughuli zingine zinazofanywa na taasisi hiyo ni kushauri namna ya kufungua kesi katika masuala ya jinai, madai, ndoa, ardhi na usimamizi wa mirathi pamoja na kuwawakilisha wateja wao mahakamani katika shauri lolote la kisheria.

Alitaja kazi nyingine ya taasisi hiyo kuwa ni kuwasaidia watu binafsi kuunda na kusajili kampuni au taasisi na kujenga uwezo wa taasisi au watu binafsi kuhusu sheria mbalimbali za nchi na kimataifa na kufanya tafiti mbalimbali kuhusu masuala ya kisheria. 

Kwa mawasiliano na taasisi hiyo wasiliana nao kwa facebook lecriconsult, twitter lecriconsult na instrag ni lecriconsult1601 na simu namba 0767855174 na 0657023585.

No comments: