JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA
RAIS
TAWALA ZA
MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI YA
MKUU WA MKOA ARUSHA
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka
Gambo amekamilisha ziara yake ya kikazi
ya SIKU
TANO mfululizo aliyoifanya katika Wilaya ya Ngorongoro yenye lengo la
kujitambulisha kwa wananchi wake, kufahamu changamoto na fursa zilizopo pamoja
na kukagua miradi ya Maendeleo.
Katika ziara
hiyo iliyokua na mafanikio makubwa Mhe. Gambo alitembelea Tarafa zote tatu
ambazoni Sale, Loliondo na Ngorongoro kwenye Kata za Ngarasero, Pinyinyi,
Oldonyosambu, Digodigo, Samunge, Olorien, Soitsambu, Ololosokwani, Piyaya,
Nainokanoka pamoja na Kata ya Endulen. Pia alifanya mikutano ya hadhara kwenye
kila kata ili kusikiliza kero za wananchi.
Aidha
kupitia ziara hiyo Mkuu wa Mkoa aliweza kukutana na wafanyakazi wa Taasisi za
Serikali zinazotoa huduma katika Wilaya ya Ngorongoro, Makapuni ya Utalii
yaliyowekeza katika Wilaya hiyo, Baraza la wafugaji, taasisi binafsi pamoja na
wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Kupitia
ziara hiyo ya kazi Mkuu wa Mkoa Mhe. Gambo alibaini na kutoa maelekezo katika
maeneo yafuatayo:
i.
Ugonjwa wa ajabu
wa kutapika damu kwa wakazi wa Kata ya Pinyinyi uliosababisha vifo vya watu 21,
ambapo Mkuu wa Mkoa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa kuleta wataalam kufanya tafiti
na kupata ufumbuzi wa tatizo hilo na mpaka ziara inamalizika wataalamu toka Wizara
ya Afya na Taasisi ya Utafiti ya magonjwa ya binadamu (NIMR) walikua
wameshafika kwenye kata hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa maagizo hayo. Pia alimuagiza
Mkurugenzi kuboresha Zahanati ya Kata hiyo iliyopo mpakani mwa Kenya na
Tanzania yenye umbali wa zaidi ya Km 120 kutoka makao makuu ya Wilaya.
ii.
Kutokuwa na mawasiliano
ya mitandao ya Simu katika Tarafa ya Sale na baadhi ya Kata za Ngorongoro; ambapo Mkuu
wa Mkoa ameahidi kukutana na makampuni ya Simu hasa yale yaliyoelekezwa kufikisha
huduma za simu maeneo ya vijijini ili waweze kufikisha huduma hiyo maramoja.
iii.
Matumizi mabaya
ya Fedha za Umma; Kutokana na hili Mhe. Gambo aliwasimamisha kazi watumishi watatu
wa Halmashauri ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhifu wa fedha za uchaguzi pamoja
na miradi mingine ya maendeleo yenye thamani zaidi ya Tsh 500 milioni. Watumishi hao ambao ni Mwekahazina Bw. Evans
Mwalukasa, Mwanasheria Bw. Sembeli Siloma pamoja na Afisa Uchaguzi Bi. Hadija Mkumbwa.
Sambamba na hilo Mhe. Gambo amezuia watendaji
wa kata kuhudhuria vikao vya Baraza la madiwani kwa kuwa si wajumbe halali wa Kikao
hicho na ambapo hadi sasa wamesababishia Halimashauri hasara ya Tsh 132 milioni. Aidha amemuagiza katibu
Tawala Mkoa wa Arusha kumuandikia Katibu Mkuu Tamisemi ili awarudishe aliyekuwa
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Ngorongoro Bw. John Kulwa Mgalula na Afisa Mipango
Bw. Louis Chambi pamoja na Mhandisi Eng.
Maziku kuja kujibu tuhuma zinazowakabili. Rc Gambo amechukua hatua hizo mara baada
ya kupokea taarifa ya kamati aliyoiunda kabla ya ziara hiyo.
iv.
Madeni ya Walimu; Mkuu wa Mkoa
aliagiza Halmashauri kulipa madeni ya walimu kwa kutuimia fedha za ndani ili kupunguza
madeni yao. Aidha Rc Gambo alishangazwa kuona Halimashauri inadaiwa Million Tatu na laki Nane na walimu wa Sekondari
Wilayani Ngorongoro na Halimashauri kusema inasubiri fedha kutoka Serikali Kuu.
Alimuelekeza Mkurugenzi Mtendaji kulipa mara moja kwa kuwa hicho kiasi ni kidogo.
v.
Usafiri wa Madiwani; Mkuu wa Mkoa
alitoa maagizo ya kusitishwa mara moja utaratibu
wa Halimashauri kutuma gari za Serikali kumfuata kila Diwani nyumbani kwake
maana taratibu hazisemi hivyo. Badala yake Mkurugenzi afanye jambo hilo kwa
kufuata Sheria na Taratibu. Pia alimuelekeza Mwenyekiti wa Halimashauri hiyo kutumia
gari ya Serikali mara mbili kwa wiki kama taratibu zinavyotaka. Aidha, fedha zitakazookolewa
kwa utaratibu huu zielekezwe katika kupunguza
madeni ya walimu wilayani hapo.
vi.
Changamoto za
huduma duni za afya, Elimu na maji; Mkuu wa Mkoa aliwataka Halmashauri kwa kushirikiana
na wadau kuboresha huduma hizo na kuhakikisha wanajenga Vituo vya Afya badala ya
zahanati ili wakina mama waweze kujifungua salama. Mhe Gambo alichangia bati zaidi
ya 500 na fedha zaidi ya Tsh Mil. 3,000,000 ili kushughulikia matatizo hayo.
Aidha, alisema hali ya usimamizi wa miradi ya Maji ni mbaya sana hivyo Halimashauri
ijipange upya kusimamia miradi hiyo.
vii.
Migogoro ya
Ardhi
inayotokana na kutopimwa kwa vijiji
hivyo na kukosekana kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi; Mhe Gambo ameagiza
uongozi wa Wilaya, kukaa pamoja na wawekezaji, Sekretarieti ya Mkoa na wadau wengine
kumaliza migogoro kwa kujadiliana changamoto hizi na kuzipatia ufumbuzi wa kudumu.
viii.
Migogoro na wawekezaji; Mkuu wa Mkoa
aliagiza wananchi kushirikishwa katika kila hatua ya uwekezaji (Bottom up
approach) ili kuwepo na maridhiano baina ya wawekezaji na wananchi wa meneo husika.
ix.
Uhifadhi hasa
katika eneo la Ngorongoro na Loliondo; mkuu wa Mkoa alitaka kuwepo mpango wa uhifadhi ambao hautaathiriwa
na mifugo wala ongezeko la idadi ya watu na kuwepo na mikakati wa kudhibiti ongezeko
la mifugo ndani ya Kreta ya Ngorongoro.
x.
Chakula cha
Njaa; Rc Gambo alisema
Serikali itakaa kuona namna bora ya kupitia matamko mbalimbali yaliyotolewa na viongozi
wa awamu iliyopita ya kuwapatia Wananchi magunia
kumi bure kwa kila Kaya ili kumaliza tatizo la njaa. Pia alisema Serikali ya
Mkoa itakaa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kuangalia namna bora ya kuboresha
mpango wa chakula cha bei nafuu kutoka NFRA.
xi.
Baraza la
wafugaji;
Mkuu wa Mkoa alisema ni muhimu baraza la hilo kufanyiwa upembuzi yakinifu katika
mambo yafuatayo:
· Kuangalia
kama Baraza hilo linafanya kazi kwa kuzingatia Sheria na Taratibu
· Kama malengo
yaliyokusudiwa kuanzisha Baraza hilo yanafikiwa
· Ufanyike
ukaguzi kwa matumizi ya Fedha walizopewa kwa kipindi cha miaka mitano maana malalamiko
ya matumizi mabaya ya fedha yamekuwa mengi.
“Ikumbukwe
kwamba Baraza Hilo la wafugaji la Ngorongoro linapewa zaidi ya TSH 2.5 Billion
kila mwaka fedha ambayo ni zaidi ya mapato ya ndani ya Halimashauri ya Ngorongoro”
alisisitiza Mhe. Gambo.
xii.
Rc Gambo pia aliagiza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kukamilisha
ahadi yake ya Madawati 2000 kwa kumalizia
haraka madawati 1500 yaliyobakia ili
kusiwe na mtoto yeyote anaye kaa chini Wilayani Ngorongongoro.
Mkuu wa Mkoa
wa Arusha alihitimisha ziara yake kwa kuwataka Madiwani na Wataalam kila mmoja kufanya
kazi kwa kuzingatia Sheria na Taratibu, pia aliahidi kuwakutanisha wadau mbalimbali
wa maendeleo ili kutafuta ufumbuzi wa haraka wa changamoto zinazoikabili Wilaya
ya Ngorongoro.
Imetolewana:
Nteghenjwa Hosseah
No comments:
Post a Comment