Thursday, October 20, 2016

Siku ya Kimataifa ya kutokomeza Umasikini ilivyofana

Kila siku ya tarehe 15 Oktoba, Dunia nzima huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Umasikini, ambapo mwaka huu kauli mbiu ya siku hiyo ilikuwa ni

‘’KUTOKA UDHALILISHAJI NA UTENGWAJI MPAKA USHIRIKISHWAJI ‘’.

Mtandao wa Dini mbalimbali kwaajili ya watoto ulimwenguni uitwao Global Network of Religion for Children (GNRC-Tanzania) wamefanikiwa kuhitimisha siku hii kwa namna ya pekee kabisa ambapo tangu tarehe 15 Oktoba wamekuwa wakiandaa matukio mbalimbali yaliyolenga kuwajengea uwezo watoto haswa wa Shule za msingi kwa kuandaa mashindano tofautitofauti kama Midahalo na Michezo ikiwa na lengo la kuwajengea watoto uwezo (capacity building) na kuwapa elimu ambayo itaweza kuwakomboa katika janga la umasikini .


Wanafunzi wa shule ya Msingi Oysterbay wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baraka Chedego kutoka GNRC -Tanzania kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu
wanafunzi wakiwa katika mdahalo
Vainess Mbaga Ofisa Elimu akitoa elimu kwa watoto
Washiriki wa Mdahalo wakisalimiana na Mama Joyce Mdachi kutoka GNRC na viongozi wengine wa shule
Mfano wa vyeti walivyotunukiwa wanafunzi kutoka na ushiriki mzuri wa siku hii ya kipekee.Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments: