Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete akizungumza katika maafali ya shule ya Sekondari Chalinze wa upande kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Bwilingu Ndg. Nassar Tamim. |
Mgeni rasmi Mh.Ridhiwani Kikwete akimpongeza mwanafunzi Athumani Mwalimu aliyefanya vizuri katika upande wa taaluma kwa kupata alama ya A katika masomo yote kwenye mtihani wa majaribio(moko) |
Mwalimu Godwin akipongezwa kwa kusimamia vizuri wanafunzi shuleni hapo. na mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Chalinze Mh.Ridhiwani Kikwete. |
Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Chalinze akiweka msisitizo katika suala la maadili mema kwa vijana na kuhakikisha kuwa wanafaulu vizuri ili kuendelea kuipa hadhi na heshima shule ya Chalinze |
Wito umetolewa kwa vijana nchini kusoma kwa bidii na
kuwekeza katika elimu ili kuweza kujikomboa na kufanikiwa katika maisha yao ya
badae.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani
Kikwete katika maafali ya shule ya sekondari Chalinze,na kuwaasa vijana kushikamana na elimu kwani ndio
mkombozi wao katika maisha.
“ili ufanikiwe katika maisha ni lazima kuweka bidii
katika masomo na kuachana na mambo yasiyo na tija katika kipindi hiki cha
masomo”,alisema Ridhiwani
Aidha Mbunge huyo amewaasa vijana kutojiingiza katika
makundi yasiyofaa katika jamii na kuongeza kuwa wapo wengi walioharibikiwa kwa
kuingia katika makundi mabaya.
"Wako waliofanikiwa kwa kutumia vizuri elimu na kuwa mfano bora kwa wengine bado mna safari
ndefu jifunzeni kutoka kwa waliofanikiwa ”,alisema Ridhiwani
Aidha Mbunge Ridhiwani alitumia nafasi hiyo kumpongeza kijana
Athumani Mwalimu aliyefanya vizuri katika mitihani yake ya majaribio kwa kupata
alama ya A katika masomo yake yote.
No comments:
Post a Comment