Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akiwapongeza washiriki waliomaliza kwa wastani mzuri wa muda, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Bi Zaibabu Ramadhani mwenye umri wa miaka 47 akiwasili Katika uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi kumalizia kilomita 21
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akisalimia na Felix
Simbu kijana wa Kitanzania aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano
ya Olimpiki nchini Brazil mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi kwa ajili ya kuhamasisha Ikungi Half Marathon 2016
Washiriki wa mbio fupi za Mita 100 wakipokea maelekezo ya Mkufunzi wa Ikungi Half Marathon 2016
Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mathias Canal akisikitika kwa kushika nafasi ya tano kwenye Mbio fupi za Mita 400
Mwanzo mgumu lakini ushiriki ni muhimu
Moja ya washiriki wa mbio fupi za mita 800 akjijiandaa kwa ajili ya kuchomoka kutafuta ushindi
Washiriki wa Ikungi Half Marathoni 2016 Kilomita 21wakichuana vikali kwenye mchezo wa Riadha
Viongozi mbalimbali waliokaa Jukwaa kuu wakifatilia kwa makini mashindano ya Ikungi Half Marathon2016
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe jinsi ambavyo washiriki wa Ikungi Half Marathon 2016 walivyokuwa wakichuana kumaliza mbio hizo za Kilomita 21
Wananchi walivyoitikia kwa wingi katika mashindano ya Ikungi Half Marathon 2016
Umakini unahitajika katika kubaini muda wa washindi
Baadhi ya watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi wakifatilia kwa makini mchuano mkali wa Ikungi Half Marathon 2016
Washindi wakipokea zawaidi zao
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwapongeza washindi wa nafasi za juu
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa nafasi za juu katika mashindano hayo
Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe
Muwakilishi wa Meneja wa mgodi wa Shanta Gold Mine Bw Elisante Kanuya akitoa zawadi kwa baadhi ya washindi
Felix
Simbu kijana wa Kitanzania aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano
ya Olimpiki nchini Brazilakihojiwa na waandishi wa Habari wawakilishi wa East Africa Radio na East Africa Televisheni
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akimpongeza Bw Elisante kanuya Muwakilishi wa Meneja wa Mgodi wa Shanta Gold Mine
Na Mathias Canal, Singida
Mashindano ya Ikungi Half Marathon yenye lengo la kuibua vipaji kwa
vijana na kuviendeleza, Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana
na kuwandaa vijana hao katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na
kimataifa yamehitimishwa hii leo na kutoa taswira nyingine ya Mashindano
ya Ikungi Marathon kwa mwaka 2017.
Mashindano hayo yalianza
Septemba 3, 2016 kwa ngazi ya Vijiji, Kata na Tarafa na hatimaye kufikia
ngazi ya Wilaya ambapo viongozi wa Wilaya za Mkoa wa Singida wametakiwa
kutafakari namna bora ya kuanzisha mchezo wa kipaombele ili kutoa
taswira ya manufaa kwa jamii ya wapenda michezo.
Mgeni Rasmi
katika kilele cha mashindano ya Ikungi Half Marathon 2016 Ambaye ni Mkuu
wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe Ameyasema hayo hii leo huku
akimsihi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuanzisha Tovuti maalumu ya Ikungi
Marathon kwa ajili maandalizi ya mbio ndefu zitakazofanyika mwaka 2017.
Mhe Mtigumwe amempongeza mkuu huyo wa Wilaya hiyo kwa kubuni na
kuanzisha mchezo huo ambao umeleta chachu na mafanikio makubwa kwa
vijana wa Mkoa wa Singida ambapo ameshauri pia kubadilisha mwezi wa
ufanyaji wa mashindano ili kila kijana apate nafasi ya kushiri ambapo
amesema kuwa mashindano hayo yamebeba taswira ya Mkoa mzima hivyo
ameahidi kuyaongeza nguvu na kutoka kwenye ngazi ya Wilaya na kuwa ngazi
ya Mkoa.
Tangu kuanza kwa Mashindano haya mwanzoni mwa Mwezi
Septemba mwaka huu vijana zaidi ya 150 walijitokeza kushiriki ambapo
kati yao vijana 60 pekee ndio walifanikiwa kuingia ngazi ya Wilaya
ambapo kati yao wanaume ni 52 na wanawake ni 8.
Kwa upande wake
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu awali akizungumza
kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa alisema kuwa aliamua kuanzisha
mashindano hayo ya Ikungi half Marathon 2016 kutokana na washiriki wengi
wazaliwa wa Ikungi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya
Riadha ngazi ya Kitaifa na Kimataifa akiwemo Bw Felix Simbu aliyeshika
nafasi ya tano kwenye mashindano ya Olimpiki nchini Brazil, Na Bi Tausi
Said aliyefanya vyema nchini Canada.
Dc Mtaturu ametumia nafasi
hiyo pia kuzitambulisha fursa zilizopo katika Wilaya ya Ikungi katika
shughuli za kiuchumi na kijamii katika kuinua kipato cha wananchi wa
Wilaya hiyo, Ikiwemo fursa za nyanja mbalimbali katika uwekezaji kama
vile Kilimo na mifugo kwa maana yauzalishaji wa mazao ya chakula kama
vile uwele, Viazi vitamu, Mahindi na vitunguu, Mazao ya biashara kama
vile alizeti na Ulezi.
Fursa zingine zilizotajwa na Mkuu huyo wa
Wilaya ya Ikungi ni pamoja na Msitu ya asili unaowezesha ufugaji wa
nyuki na kupata asali bora, Ardhi na maji kwa uwepo wa maeneo chepechepe
kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na mazao ya bustani lakini pia
uchimbaji wa madini wakiwemo wachimbaji wadogo na wachimbaji wakubwa.
Mhe Mtaturu pia alisema kuwa uwepo wa mkondo wa upepo kwa ajili ya
uzalishaji wa umeme wa upepo katika vijiji vya Unyankanya na Siuyu
Tarafa ya Mungaa.
Dc Mtaturu amesema kuwa Wilaya ya Ikungi
imedhamiria kwa dhati kuwekeza katika michezo kwani itakuwa chachu kwa
wawekezaji, Sambamba na kutoa fursa kwa wananchi wake hasa katika
kuongeza kipato, Kutoa ajira na kupandisha taaluma ya michezo kwa wakazi
wa Wilaya ya Ikungi na Mkoa wa Singida kwa ujumla.
Naye Felix
Simbu kijana wa Kitanzania aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano
ya Olimpiki nchini Brazil ameiomba serikali kuwaandaa vijana kwa ajili
ya mashindano
No comments:
Post a Comment