Saturday, October 22, 2016

RC GAMBO APOKEA MSAADA WA BATI 500 NA MIFUKO YA SARUFI 500


Mhandisi wa Wakala wa barabara Mkoa wa Mkoa John Kalupale (kwanza kulia) akiwatambulisha wawakilishi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd walipokuja kukabidhi msaada wa mabati na Cement kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Maneja Mradi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, Bw.Xie (kulia mbele) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (mbele kushoto) mfuko wa saruji na bati kama sehemu ya msaada wa bati 500 na mifuko ya saruji 500 waliyoitoa kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za Maendeleo katika Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo (mbele) akishukuru Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd kwa kutoa msaada kwa wananchi wa Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo(mbele kushoto) akikabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha mifuko ya saruji 100 na bati 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha kupitia Tiket ya Ccm Catherine Magige(kwanza kushoto) akitoa shukrani kwa kampuni ya Ujenzi iliyotoa msaada kwa ajili ya kuwezesha huduma za kijamii Mkoani Arusha.
Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Kundi la Walemavu kupitia Tiket ya Ccm Amina Mollel(kwanza kushoto) pia alitoa shukrani zake kwa kwa Kampuni iliyotoa msaada.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia (pili kulia) akishkuru kwa msaada wa Mabati 100 na Mifuko ya saruji 100 aliyopewa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Terrat.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kushoto) akimshkuru Meneja wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, baada ya kuhakiki msaada wa mabati 500 na mifuko ya saruji 500.
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Mhe. Catherine Magige baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati 500 na mifuko ya saruji 500 toka kampuni ya ujenzi wa barabara ya Sakina Tengeru na barabara ya Mchepuko.

…………………………………………….

Nteghenjwa Hosseah – Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepokea msaada wa bati 500 pamoja na mifuko ya saruji 500 kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati pamoja na shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Arusha.

Mara baada ya kukabidhi wa msaada huo nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu huyo, Gambo alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Dararro mifuko 100 ya saruji na mabati 100 kwa ajili ya ujenzi kituo cha afya kinachojengwa eneo la kwa mama mbauda kata ya Muriet Jijini Arusha.

Alisema msaada huo utawezesha kila wilaya kunufaika nao kwani kila wilaya za mkoa wa Arusha kuna changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na mahitaji ya majengo ya zahanati ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Alimshukuru Meneja Mradi wa Kampuni ya ujenzi ya Hanil – Jiangsu Joint Venture Ltd, inayojenga barabara ya Sakina – Tengeru Km 14.1 na barabara ya Mchepuko Km 42.4 , Xie Jianbao ambao wametoa msaada huo kama sehemu ya kurudhisha kwa jamii ya watanzania ili kukuza mahusiano na kujali jamii na Taifa ambalo limewapa kazi kubwa ya ujenzi wa barabar hiyo itakayogharimu takribani Bil. 139.

“Naishukuru kampuni hii kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya kuleta maendeleo na naahidi tutautumia ipasavyo katika kuleta maendeleo na kila wilaya nitakayofanya ziara msaada huo nitaupeleka ili ya kupunguza changamoto mbalimbali kwa jamii “.

Naye Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Bw. Xie alisema kampuni yao imeona umuhimu wa kuchangia jamii kwani wao ni wajenzi wa barabara na wanastahili kurejesha faida kwa jamii inayowazunguka.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro alimshukuru Gambo kwa msaada huo na kusisitiza kuwa mifuko hiyo 100 ya saruji pamoja na bati 100 zitasaidia ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa Kata ya Muriet Jijini Arusha.


Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alishukuru kwa msaada huo utakaosaidia ujenzi wa kituo cha afya kujengwa na kukamilika ndani ya miezi miwili na kuahidi kwamba atasimamia ipasavyo ili kuhakikisha Kituo kinajengwa katia ubora unaostahili.

Katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na wabunge wa Viti maalum wanawake Mkoa wa Arusha, Catherine Magige na Aminah Mollel walitoa rai kwa nyakati tofauti kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kumuunga mkono Mhe. Gambo pamoja na Serikali ili kuwezesha maendeleo kusonga mbele.

No comments: