Naibu
Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya
(kulia) akikata utepe wakati uzinduzi wa program ya JIANDALIE AJIRA
inayolenga kupunguza tatizo la ajira nchini. Wengine katika picha ni
Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kimataifa wa Vijana (IYF), Bw.
William Reese (wa pili kulia), Mwenyekiti wa bodi wa Taasisi ya
Ujasiriamali na Ushindani TECC Bi. Beng’I Issa (kushoto), Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani, Bw. Sosthenes Sambua
(wa pili kushoto) na Ahmed Makbel Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira kutoka
ofisi ya Waziri Mkuu (katikati).
Rais
na Afisa Mtendaji Mkuu wa wa Mfuko wa Kimataifa wa Vijana (IYF), Bw.
William Reese, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya
Jiandalie Ajira jana jijini Dar es Salaam, wengine katika picha ni
Mwenyekiti wa bodi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) Bi.
Beng’I Issa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa (TECC) Sosthenes Sambua
katikati, program hiyo ili zinduliwa na Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi
na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya kwenye ukumbi wa kimataifa wa
Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana.
Na Ally Daud-MAELEZO.
Mfuko
wa Kimataifa wa Vijana( Interanational Youth Foundation) imezindua
rasmi programu mpya ya miaka mitano wa JIANDALIE AJIRA unaowalenga
vijana hapa nchini kama moja ya jitihaha za kukuwajengea vijana mafunzo
ya ufundi stadi na ujasiriamali kuondokana na tatizo la ajira .
Akizindua
programu hiyo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Technolojia ,Mhandisi
Stella Manyanya alisema program hiyo ni ukombozi mkubwa kwa vijana hapa
nchini kwa kuwa itawawezeshae kutengEneza ajira na kukuza uchumi.
“Programu
hii imekuja kutengneza vijana kuwa wabunifu na kutengneza ajira ikiwa
ni pamoja na kuajiri wengine na siyo kuwa wasaka ajira,”na kwa kufanya
hivyo taifa litapiga hatua kiuchumi,aliongeza kusema,Mhandisi huyo
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa” alisema Mhandisi Manyanya
Aidha
Mhandisi Manyanya aliupongeza mfuko huo wa IYF kwa kuja na mradi ambao
utatekelezwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Ujasirimali na Ushindani
(TECC), Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Shirika lisilokuwa la
kiserikali la The MasterCard Foundation.
Mhandisi
Manyanya alisema pia programu hiyo itawezesha kuwaandaa wakufunzi wa
chuo cha VETA ili waweze tumika katika kuwafundisha vijana ambao ndio
walengwa katika mradi mzima na ambao wanachangamoto kubwa ya ajira.
Mbali
na hayo Mhandisi Manyanya alikitaka chuo hicho kuendeleza na kupanua
wigo wa ushirikiano na waajiri ili kujenga nguvu kazi kukidhi matwakwa
ya soko la ajira kwenda sambana na dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka
2025.
Kwa
upande wa Rais wa IYF ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa mfuko huo
Bw.William Reese alisema mfuko wao umeandaa mpango huo kwa nchi za
Tanzania na Msumbiji kwa ajili ya kuwaandaa vijana katika elimu ya
mafunzo ya ufundi stadi na uujasirimali
“Tatizo
la ajira siyo la Tanzania tu bali la dunia nzima kwa nchi zilizoendelea
na ambazo hazijaendelea”, na hitaji mipango ya pamoja, ya kidunia na
yakinchi kwa kushitrikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali”
alisema Bw. Reese.
Pia
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika IYF (Regional Director,Africa) ,
Bw.Mathew Breman alisema mpango wa jiandallie ajira utaendeshwa kwa muda
wa miaka mitano na unalenga kuwapatia mafunzo ya ufundi stadi na
jasirimali kwa vijana.
”
Programu hii inahusu vijana wa miaka 18 hadi 24 na watapata mafunzo na
mikoa inayolengwa ni pamoja na Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara,na
Morogoro,” na vijana 22,500 watanufaika na mradi huu, aliongeza Bw.
Breman.
Aidha
Bw. Breman mradi unaletekezwa katika nchi Msumbiji ambapo kwa pamoja na
Tanzania utanufaisha vijana 30,000 kupata mafunzo ya ufundi stadi na
ujasiriamali katika kipindi hicho.
Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Ujasirimali na Ushindani (TECC),Bi. Issa Beng’I alisema program hiyo ni muhimu kwa vijana.
“Tunazo
program nyingi hapa nchini Tanzania, ikiwemo kijana jiajiri, vijana wa
bodaboda,vijana wa JKT, na sasa program ya jiandalie ajira itawawezesha
kujitambua zaidi,” na kufanikiwa kwa hili ni ukombozi mkubwa kwa taiafa
letu, aliongeza kusema Bi. Issa.
Moja
ya vijana , Nuru Mungi akitoa ushuhuda wa biashara yake, alisema
mafanikio aliyoyapata katika ujasirimali yamekuja baada ya kupata
mafunzo (TECC).
“
Kutokana na mafunzo haya sasa namiliki kiwanda kidogo cha kutengneza
sabuni na naamini kupitia program ya jiandalie ajira vijana wengi
watanufaika na kupanua wigo wa ujasirimali.alisema.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Ajira toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ahamed Makbel,alisema
tatizo la ajira hapa nchini kwa kwa sasa limefikia asilimia 10.3.
“Tatizo
hili kwa vijana limefikia asilimia 11.7 kwa vijana amabyo ni nguvu kazi
kubwa inayobeba asilimia 56 kwa nchi nzima, vijana hao wanaumri kati ya
miaka 15 hadi 35.
Mfuko
wa IYF umesha fanya kazi katika mataifa zaidi ya 70 duniani ili kuweza
kusaidia vijana mbalimbali kwa ajili ya kukuza uchumi wa kijana na taifa
kwa ujumla ili kufikia uchumi wa kati.
No comments:
Post a Comment