Friday, October 21, 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI AZINDUA KITUO KINACHOTOA HUDUMA ZA MAGARI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Hamad Masauni, akikata utepe kuashira ufunguzi wa kituo kipya cha kisasa cha huduma ya magari madogo na makubwa kilichopo Magomeni Mwembe chai jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, Kushoto ni Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani ,Mohamed Mpinga na Meneja usambazaji kanda ya Afrika Mashariki Dkt.Fulgence Bube.
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, akimsikiliza kwa makini,Naibu waziri wa mambo ya Ndani ,Mhandisi Hamad Masauni katika hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha kutoa huduma kwa magari makubwa na madogo kilichopo Magomeni Mwembe Chai jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Superdoll Tanzania ,Seif .A. Seif, akizungumza na wadau waliofika katika uzinduzi wa kituo kipya cha huduma kwa wateja.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Mhandis Hamad Masauni, akizungumza na wadau waliofika katika uzinduzi wa kituo cha wateja.
Wadau wa mbalimbali wa masuala ya usafirishaji nchini wakifuatilia uzinduzi uzinduzi huo.
Msimamizi wa kituo cha kutoa huduma za magari cha Mwembechai akitoa maelezo kwa waziri na viongzi mbalimbali.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Superdoll wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa kituo cha kisasa cha kutoa huduma ya magari makubwa na madogo kilichopo Magomeni mwembe chai jijini Dar es Salaam.Picha zote na Humphrey Shao wa Globu ya Jamii



Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

Watanzania wanaotumia vyombo vya moto wametakiwa kufanya uchunguzi wa mara kwa mara kabla ya kuanza safari ili kuweza kupunguza ajali za barabarani.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Kisasa cha kutoa huduma ya magari makubwa na madogo kilichopo Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam,Masauni amesema kuwa kufanya uchunguzi wa magari katika kituo hicho kitasaidia kupunguza ajali za barabarani.

Amesema teknolojia inakua kwa kasi hivyo magari ya sasa yanatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kisasa kabla ya kuanza kwa safari katika kituo cha mwembe chai.Masauni amesema Superdoll wamekuwa wabunifu wa teknolojia ya kisasa ya katika vyombo vya moto ikiwa ni kuweka safari kuwa salama kwa safari zote.

Amesema kuwa kunzisha kituo hicho watakuwa wamesaidia ujenzi katika masuala ya usalama barabani na kuweza kupunguza ajali za barabarani.Masauni amesema kuwa watashirikiana na superdoll na kampuni ya matairi ya Michelin katika kufanya uchunguzi wa magari kwa teknolojia ya kisasa

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabani, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi, Mohamed Mpinga, amesema superdoll wamekuwa wadau wa usalama barabarani na kuendelea kuwa wabunifu katika teknolojia mbalimbali.

Amesema wanaomiliki vyombo vya moto watumie kituo cha uchunguzi wa teknolojia ya katika kuweza usalama wa gari na maisha watu katika kufikia lengo la serikali ya kupunguza ajali barabarani.

Mkurugenzi wa Superdoll, Seif Seif amesema kuwa kuna tayari zimekuwa zikiingizwa nchini ambazo matumizi yake ni kwa nchi zenye barafu wakati Tanzania hatuna uhitaji wa hizo.

No comments: