Tuesday, October 25, 2016

MATUKIO MBALIMBALI UFUNGUZI WA MKUTANO WA KIUCHUMI WA KOREA NA AFRIKA MJINI SEOUL, KOREA KUSINI

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akionesha kitabu alichozawadiwa na kuelezea umuhimu wake kwa nchi za Kiafrika kukisoma na kukielewa kitabu hicho ili ziweze kuiga mbinu ambazo nchi hiyo imezitumia hadi kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kiuchumi duniani.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (Katikati) akiwa na ujumbe wa maafisa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango makao makuu, TRA Tanzania Bara na Zanzibar, Ofisi ya Mwanasheri Mkuu wa Serikali, wanaoshiriki kujadili mkataba wa kuepusha kutoza kodi mara mbili kwa raia wa nchi mbili za Tanzania na Korea, wakiwa mjini Seoul, Korea Kusini.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Grand Intercontinental, Seoul Parnas, Korea kwaajili ya ufunguzi wa mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEK), Mjini Seoul, Korea Kusini.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akibadilishana mawazo na maafisa kutoka Tanzania kabla ya kuanza kwa mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Kiafrika( KOAFEC), uliofanyika mjini Seoul Korea Kusini. Katikati ni Mkuu wa idara ya kutafuta rasilimali kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Sabra Issa Machamo  na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa  TANESCO, Decklan Mhaiki.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akibadilishana mawazo na watendaji wakuu wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini Kabla ya kufunguliwa Rasmi kwa Mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), unaofanyika Mjini Seoul, Korea Kusini.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na wapili kushoto, akiwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Korea Kusini, Yoo II Ho (kushoto kwake) na Rais wa Benki ya EXIM-Korea, Lee Duk-Hoon (Kulia kwa Waziri), kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), katika ukumbi wa Grand Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini.
 Mawaziri wa Fedha kutoka nchi 54 za kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Tano wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi Afrika (KOAFEC) wakiweka alama ya kiganja cha mkono kwenye kibao chenye malighafi maalumu yanayoshika alama za vidole kuonesha ushirikiano na umoja, baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano huo katika ukumbi wa  Grand Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa ameshika kibao alichoweka alama ya kiganja chake, kuunga mkono umoja na mshikamano wa nchi za Kiafrika zinazohusiana kiuchumi na Korea Kusini baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa Tano wa ushirikiano huo kati ya Korea Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC) katika ukumbi wa Grand Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (Katikati) (Kulia kwake) na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Akinwumi Adesina, (Kushoto) Baada ya kufunguliwa Rasmi kwa Mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Kiafrika, unaofanyika Mjini Seoul, Korea Kusini
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa na Maafisa kutoka Tanzania, wakitoka kwenye Ukumbi wa Mikutano  wa Grand Intercontinental, Seoul Parnas, Korea Kusini, baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Afrika, mjini Seoul, Korea.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Mpango (Mb), akipokea zawadi ya kitabu kinachoelezea njia zilizotumiwa na nchi ya Korea Kusini, kupiha hatua kubwa ya maendeleo, kutoka kwa Afisa Mikopo wa Benki ya Exim ya Korea Kusini, Park Gil Jong, kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa tano wa ushirikiano wa Korea Kusini na nchi za Afrika  (KOAFEC), Mjini Seoul, Korea Kusini. Picha zote na Benny Mwaipaja-WFM (Wizara ya Fedha na Mipango

No comments: