Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu
cha wageni Ikulu Ndogo Mkoani Morogoro.
|
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akicheza ngoma
ya asili na baadhi ya viongozi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji
maalum ya Fungafunga
|
Kaimu Afisa Mfawidhi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw.Rashid Omar akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli hotuba. |
Baadhi
ya Wazee wakimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama
Janeth Magufuli
|
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi
ya kuku kutoka kwa mmoja wa kiongozi wa makazi ya wazee ya Fungafunga.
|
Baadhi
ya Nyumba Wanazoishi wazee katika Makazi ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya
Morogoro.
|
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akibadilishana
mawazo na mmoja ya wazee katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji
maalum ya Fungafunga
|
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga |
Wizara,
Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau
mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu
wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri
iwekenavyo.
Hayo
yamesemwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakati akiongea na wazee na watu
wenye ulemavu alipotembelea kituo cha wazee na watu wenye mahitaji maalum cha
Fungafunga kilichopo Mkoani Morogoro.
“Kundi
hili ni moja kati ya makundi yaliyokatika hatari kubwa sana na kwa kiasi
kikubwa ni kundi ambalo limekuwa likisahaulika sana na kuwafanya kukosa
mahitaji muhimu wanayopaswa kuyapata hivyo rai yangu kwa Wizara, Taasisi za
Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa
maendeleo kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili
kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu”. Alisema Mama Janeth.
Pia
Mama Janeth alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.
John Pombe Magufuli inatambua kuwa wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika
kukuza uchumi wa nchi hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau
mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote
muhimu.
Aidha,
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa Mchele kilo 875,Unga Kilo 875, Sukari
Kilo 175, Maharage Kilo 350 na Mafuta ya
watu wenye ulemavu wa ngozi boksi 1 Mama Janeth aliwataka viongozi wa kituo
hicho kuhakikisha chakula hicho kinawafikia walengwa kama ilivyopangwa.
Akiongea
wakati akimkaribisha Mama Janeth Magufuli, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi.
Regina Chonjo aliwataka ameataka viongozi wa kituo hicho kuwasiliana mara kwa
mara na viongozi wa mkoa pale wanapohitaji msaada ili kusaidia kuondoa
changamoto zinazowakabili wazee katika kituo hicho.
Naye
Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo hicho Bw.Rashid Omar alimshukuru Mama Janeth
Magufuli kwa uamuzi wake wa kuja kukitembelea kituo hicho kwani ni faraja kwa
wazee na watu wenye ulemavu hasa kwa kupokea msaada wa chakula.
No comments:
Post a Comment