Friday, October 21, 2016

MAHAFALI YA 13 YA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARI BWAWANI YAFANA MKOANI PWANI

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akisalimiana na mmoja wa wazazi alipowasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Bwawani kushiriki Mahafali ya 13 ya Shule hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa Kidato cha nne katika Mahafali ya 13 ya Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.
Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya hotuba ya Mgeni rasmi.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akitoa neno kwa wahitimu katika Mahafali ya 13 ya Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.
Wahitimu wa Kidato cha Nne wakitoa burudani ya Wimbo Maalum wa Shule hiyo.
Meza Kuu wakiimba wimbo wa Shule ya Sekondari Bwawani kama wanavyoonekana katika picha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya akizindua rasmi Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Bwawani wakati wa Mahafali ya 13 ya Kidato cha nne.
Muonekano wa Bweni la Wanawake lililokamilishwa kujengwa tayari kwa matumizi katika Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.
Muonekano wa ndani wa Bweni la Wanawake lililokamilishwa kujengwa tayari kwa matumizi katika Shule ya Sekondari Bwawani, Mkoani Pwani.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Kidato cha Nne(waliosimama) katika Mahafali ya Shule ya Sekondari Bwawani(wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja.(Picha zote na Jeshi la Magereza).

No comments: