Sunday, October 9, 2016

KKKT DAYOSISI YA IRINGA YAPATA ASKOFU MPYA

Askofu  wa kanisa la  kiinjili la  Kilutheri  Tanzania (KKKT)  dayosisi ya  Iringa Dkt  Owdenburg Mdegela katikati  akiwatambulisha  mbele ya waumini wa kanisa  kuu  askofu  mteule wa dayosisi  hiyo mchungaji  Blaston  Gavile (wa  pili kushoto)   na mkewe  pamoja na msaidizi wa askofu huyo mchungaji Himid Saga  (wa pili  kulia)  na mkewe
Askofu wa Dododa Mwamasika kushoto  akiwa na askofu mteule wa  dayosisi ya  Iringa Blaston Gavile na mkewe wakimsikiliza askofu wa dayosisi  hiyo Dkt Mdegela
Katibu  wa dayosisi ya Iringa Chavala  kulia  akimfuatilia kwa makini askofu wa Dodoma
Askofu  Mwamasika  kulia  akimpongeza mke wa askofu mteule wa  dayosisi ya  Iringa katikati ni askofu Dkt Mdegela
Mchungaji wa usharika wa kanisa  kuu  Mbogo  akiweka sawa  mic 
Askofu  wa  doyosisi ya  Iringa Dr Mdegela  kulia  akimtambulisha rasmi askofu mteule wa dayosisi hiyo mchungaji Blaston Gavile na mkewe mbele ya  waumini wa kanisa kuu leo
Askofu  Dkt Mdegela  akitoa maelezo kwa waumini  wa kanisa kuu
Mmoja  wa  wageni  akimpongeza askofu dkt Mdegela  kwa kufanya uchaguzi wa  kihistoria
Viongozi wa kwaya ya  vijana  wakiwa katika  picha ya pamoja
Mwalimu  wa kwaya ya  vijana Lupyana Samweli  kulia  akimpongeza askofu Dkt Mdegela
Askofu  Dkt Mdegela  akiwa na wanandoa  watarajiwa kulia ni Debora  Lubava mtunza hazina  wa kwaya ya  vijana na  ubavu wake mtarajiwa  kulia
Askofu Dkt Mdegela  akihoji  jambo kwa  mwimbaji wa kwaya ya vijana Onno Mella

Na Francis Godwin
ASKOFU  wa  kanisa la  Kiinjili la  Kilutheri  Tanzania (KKKT)  Dayosisi ya  Iringa  Dkt. Owdenburg Mdegela amewapongeza  waumini  wa Dayosisi   hiyo kwa kumpata  askofu  mpya  atakayechukua  nafasi  yake pasipo  kuwepo  kwa  vurugu  za aina   yoyote  tofauti na maeneo  mengine  ambayo pindi  linapotokea  zoezi  la uchaguzi wa askofu huwa na vurugu kubwa .

Huku akisema   kuwa  hana  ugomvi wowote  na askofu  wa  Dayosisi Kusini Isaya  Mengele kama  ambavyo  watu  wanasema na  kuwa mgogolo  unaoendelea  kati ya askofu    huyo  na  waumini  wake  wa  jimbo la Mufindi utatuzi  wake ni maombi na  sio  kutumia  nguvu. Alisema tayari  amepokea maombi  ya  waumini wa  jimbo la Mufindi  kutaka  kuhamia  dayosisi ya Iringa na hana sababu ya  kuwakataa  kuwa  pindi  watakapokuwa tayari atawakaribisha.
Askofu Dr  Mdegela  aliyasema  hayo leo  wakati wa ibada  maalum  ya  kumtambulisha  Askofu  mteule Mchungaji Blaston Gavile  na msaidizi   wake Himid Saga  mbele ya  waumini wa kanisa  hilo  Usharika  wa Kanisa  kuu, kuwa  uchaguzi mkuu  uliofanyika Ijumaa umemalizika  kwa amani  na  utulivu  mwingi  na  kupelekea heshima  kubwa kwa dayosisi ya Iringa na Tanzania kwa  ujumla.
" Tumemaliza  uchaguzi   wetu kwa amani na  utulivu  mwingi na hadi  sasa hapa  nimepokea salamu  za  pongezi  kutoka Dayosisi  mbali mbali na hata  nje ya  Tanzania   wakipongeza kwa  jambo   hilo  kufanyika pasipo kuwepo kwa  vurugu  zozote ....hii  ni  heshima  kuwa imewekwa na  yote haya  yamewezekana  kutokana na kazi nzuri ya  waumini  kufanya maombi "

Alisema   kuwa  hakuna  jambo  lolote  alilolifanya vema  pasipo   kumtanguliza  roho  mtakatifu  hivyo  ombi  lake  kwa wale  waliopewa kazi na Mungu ya  kuongoza dayosisi hiyo  ni kuepuka  kusikiliza  maneno ya   watu  wanayoyasema barabarani  na  badala  yake  kumtanguliza  Mungu na  kusikiliza  kile  kinachosemwa na  viongozi  wa dayosisi  kwani  maneno ya mitaani  ni  ya  hivyo  hivyo.

"  Mimi yamesemwa  mengi ila nawasamehe   bure   wale  wote  waliosema ila nawaomba baadae  wote  wakatubu wapo  ambao walikuwa  wakifanya kazi ya  kunichafua katika   vyombo  vya  habari na mitaani kwa kusema mambo ya aibu dhidi  yangu ila kiuharisia sivyo   hivyo ....kuna  wengine ni maaskofu  walipata  kutamka  kuwa  mimi natumia vibaya  fedha  za  chuo kikuu  cha  Iringa wakati  wao ni  wasomi na  wanajua  kabisa  kuwa chuo  kinakaguliwa na  kuna taratibu  nzuri  tu  za  kifedha ila kwa  kuwa walikuwa wanafanya  hivyo kwa kufurahisha  nafsi  zao na  kupotosha nasema  ni  wakati wa  wote kutubu na  wakitubu waje  kuniomba msamaha "
Akifafanua  juu ya ajenda  ya  waumini  wa Kanisa  hilo jimbo la Mufindi  kutaka  kuhama  Dayosisi yao ya Kusini  na kuhamia  Dayosisi ya  Iringa  alisema  kuwa  kuwa ajenda   hiyo  ilizungumzwa na aliyewasilisha ajenda  kwenye  mkutano  mkuu huo  alikuwa ni  yeye  mwenyewe.

" wapo  watu  wanapotosha  kuwa ajenda  ya  Mufindi  kuhamia Dayosisi ya  Iringa hakuzungumzwa  kwenye mkutano mkuu nawaambia  kuwa ajenda   hiyo  imezungumza na mimi  ndie  niliyeiwasilisha  usiku  wa octoba 6  mbele ya  wajumbe  kwa  kutoa  maelezo maana ajenda  ya askofu ni  ajenda  ya  mkutano  mkuu  hivyo  sikuipeleka  Halmashauri  kuu  wala  kamati ya  utendaji   nilitoa  taarifa  kwenye  mkutano  huo  kuwa Mufindi  wameamua  kuhamia Iringa  tulipowauliza  kuwa  wanataka  dayosisi  walisema  hapana  wao  wameamua  kuhamia Dayosisi ya Iringa  hivyo  niliwaambia  wajumbe  kuwa  hamuwezi ninyi  kuwaambia  wasihamie  maana dayosisi  ni  mali ya  Mungu si mali ya  mwanadamu na  wakihamia  kuhamia popote  wao  wanaweza hivyo  wajumbe wa mkutano  huo  walikubali  kuwapokea ..... hoja  ya pili wajumbe  walisema  kutokana na  jambo  hilo  kuwa  bado  linasumbua  kanisa  waliniomba  mimi Mdegela  kuendelea  kuliratibu jambo  hilo  hadi  mwisho  ila  kuna  uzushi  umetokea  kuwa  katibu  mkuu  anasema ajenda  hiyo haikuwepo ni kweli kabisa ajenda kubwa  ilikuwa ni uchaguzi mkuu lakini  ile  nilisimama  nikasema kama  mimi kwa  hiyo mimi nawajibika  kusema mbele  ya  wajumbe na  pia  nawajibika  kubaki na  majibu ya ule  mkutano mkuu yanayosema  maamuzi ya  waumini wa Mufindi ndio  tutakaouheshimu  ndio kauli ya mkutano mkuu "
Askofu  Dkt  Mdegela  alisema  kuwa watu wanasema  kuwa  msemaji wa dayosisi ya  Iringa ni katibu mkuu wapo  hao ni  wapotoshaji na  wanapaswa  kupuuzwa  kwani  hadi   sasa  yeye  Askofu ni msemaji  mkuu wa  dayosisi ya Iringa hadi hapo  januari  mwakani siku  ambayo  askofu  mpya  atasimikwa  rasmi  japo katibu  mkuu  anapaswa  kusema  kwa ruksa  kutoka  kwake hivyo anawataka  waumini wa jimbo la Mafinga  kupokea majibu ya maombi  yao kuwa yamepokelewa rasmi.
  Alisema  kuwa  waumini wa Mufindi waliomba  kuhamia dayosisi ya  Iringa baada ya  kudai kuwa hawapendi kuendelea  kubaki dayosisi ya kusini na  hivyo  walikuwa  njia panda kwanza iwapo  wangekataliwa Irinda  walipanga  kuanzisha kanisa  lao ama  kuanzisha dayosisi yao lakini  si  kubaki dayosisi ya Kusini.
" Mimi  ni mtaalam wa Imani hivyo niliwajibu  kwa  barua  kuwa cha kwanza kuwapatanisha na katibu mkuu na  askofu  wa  dayosisi ya  kusini   pia  kuombana msamaha  pale  walipokosana  ......mimi  sina  chuki  hata  kidogo na askofu  mwenzangu wa  kusini  Mengele  amekuwa ni  rafiki  yangu  siku  zote   walipokosana wakristo  wa Mufindi na askofu  wao Mengele ni pale  walipokamatwa na  kuwekwa mahabusu  kijiji  cha Mdandu na  kunyimwa  dhamana na kukosa  kushiriki mkutano mkuu  ambayo ni mamlaka  kuu ya  dayosisi na Halmashauri  kubaki  kimya  juu ya  suala  hilo sasa  mimi  nasimamia  ukweli  kuwa  mimi kama askofu sikutumwa kufunga  watu polisi nimetumwa  kuwakomboa  wakristo ndio  wanaochagua  viongozi na  wanayohaki ya  kusikilizwa sio  kufungwa gerezani  sasa  kama  haya  yanamkwaza  mwenzangu  sina  jinsi  huu ndio  ukweli  lakini tujiulize kama  Yesu  angewakuta pale mahabusu mdandu  angefanya  nini "

No comments: