Tuesday, October 11, 2016

Kiwanda cha Chaki Wilayani Maswa chaahidiwa mkopo wa shilingi milioni 30 kutoka mfuko wa vijana

Na Genofeva Matemu – WHUSM
Vijana nchini wametakiwa kuiga mfano wa vijana wa Maswa Youth Family kuunganisha nguvu zao kuibua miradi yenye tija kwani heshima ya kijana ni kujitengemea na kulitegemeza taifa lake.
Hayo yamesema na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ufunguzi wa Kiwanda cha Chaki Jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu.
“Vijana wa Maswa Youth Family ni mfano bora wa kuigwa kwani ni vijana waliojitambua na kutambua yakua umoja ni nguvu hivyo kuchagua fungu lililo jema na kuwa mfano bora kwa wana Maswa na taifa kwa ujumla” alisema Mhe. Jenista.
Aidha Mhe. Jenista amemuagiza Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kuwakopesha tena vijana wa Maswa Youth Family shilingi milioni thelathini kutoka katika mfuko wa vijana ili kiwanda hicho kiweze kukua kwa haraka na kuzalisha chaki kwa wingi hivyo kuweza kuzuia soko la chaki zinazotoka nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha chaki Wilayani Maswa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa hadi sasa uzalishaji wa chaki unaofanywa na kiwanda kidogo cha Maswa Youth Family unatosheleza mahitaji ya chaki kwa shule zote za Mkoa huo na kuzipiga marufuku shule zote mkoani hapo kununua chaki nje ya Mkoa wa Simiyu.
“Simiyu imedhamiria kuionyesha nchi kuwa sisi ngozi nyeusi tunaweza tukaibua miradi, tukajenga uwezo na baadaye tukazalisha kwa kuiendeleza kauli mbiu ya mkoa wetu ya bidhaa moja wilaya moja ambayo baadaye itashuka hadi kuwa bidhaa moja kijiji kimoja na kulifanya taifa letu kuwa taifa la viwanda” alisema Mhe. Mtaka.
Aidha Naibu Waziri Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa Mkoa wa Simiyu umekua wakwanza kuiishi kwa vitendo falsaga ya bidhaa moja wilaya moja na kuahidi kuiunga mkono falsafa hiyo kujitolea kuwa balozi wa Chaki inayotengenezwa na Maswa Youth Family ili kuweza kuitangaza nchi nzima.
Naye Mwenyekiti wa Maswa Youth Family Bw. Kelvin Steven amesema kuwa kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha chaki 38,400 kwa saa sawa na katoni 16 na iwapo uzailishaji utafanyika kwa saa nne kiwanda kitazalisha katoni 128 kwa siku na uzalishaji huo kwa siku 20 unategemewa kuwa katoni 2560 ambapo mahitaji kwa mwezi kwa Wilaya inakadiriwa kuwa katoni 157 hivyo kuwa na zaidi ya katoni 2403 ambazo zitauzwa maeneo mengine.
Mradi huu umegharimu jumla ya shilingi 37,967,522 kati ya fedha hizo shilingi 30,967,522 ni mchango wa Halmashauri na shilingi 70,000,000 ni mchango wa kikundi uliotokana na fedha za mkopo waliopewa kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe (aliyesimama kushoto) baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akipokea taarifa fupi ya Wilaya ya Maswa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Seif Shekalaghe (kushoto) baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akizungumza na viongozi kutoka Mkoa wa Simiyu na Halmashauri ya Maswa baada ya kuwasili katika Halmashauri hiyo jana Mkoani Simiyu kabla ya kwenda kufungua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (wapili kulia) akiwasili katika kiwanda cha chaki kijulikanacho kwa jina la Maswa Youth Family jana katika Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu kwa ajili ya kukizindua kiwanda hicho rasmi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na watatu kulia ni Mwenyekiti wa kiwanda hicho Bw. Kelvin Steven.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (watatu kulia) akipata taarifa fupi ya kiwanda cha Maswa Youth Family kutoka kwa Mwenyekiti wa kiwanda hicho Bw. Kelvin Steven (kulia) baada ya kuwasili katika kiwanda hicho kwa ajili ya kukizindua rasmi jana katika Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu. Wapili kulia ni Naibu Waziri Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde na kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akimimina mchanganyiko wa mahitaji ulioandaliwa kwa ajili ya kutengeneza chaki katika moja ya mashine ya kutengeneza      
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiangalia chaki zilizotengenezwa  katika kiwanda cha Maswa Youth Family kabla ya kukizundua rasmi kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na kulia ni kijana kutoka Maswa Youth Family Bw. Razaro Zabroni 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Dkt. Seif Shekalaghe (kushoto) kukata utepe kuzindua rasmi kiwanda cha chaki cha Maswa Youth Family  jana katika Halmashauri ya Maswa Mkoani Simiyu.
 
 Naibu Waziri Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde akizungumza na vijana wa Maswa Youth Family pamoja na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa baada ya uzinduzi wa kiwanda cha chaki jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dkt. Titus Kamani
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na vijana wa Maswa Youth Family pamoja na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa baada ya uzinduzi wa kiwanda cha chaki jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (aliyesimama) akizungumza na vijana wa Maswa Youth Family pamoja na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa baada ya kuzinduzi wa kiwanda cha chaki jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu. Kulia ni Naibu Waziri Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dkt. Titus Kamani
 Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) baada ya kukizindua kiwanda cha chaki kinachoendeshwa na vijana wa Maswa Youth Family jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na vijana wa Maswa Youth Family na baadhi ya viongozi waliojumuika naye katika uzinduzi wa kiwanda cha chaki jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu.

No comments: