Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba akizungumza na wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya
kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani
ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya
Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba ( wa kwanza kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni hiyo na wateja kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya
Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho
ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias
Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba (kushoto) akimsikiliza mmoja wa wateja wa kampuni ya
TTCL mwenye asili ya China juzi kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya
Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho
ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania
(TTCL), Peter Ngota akizungumza na wateja wa kampuni ya TTCL kwenye
hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika
ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja
vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya
TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo
lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma
kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya
Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya
TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo
lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma
kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya
Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania
(TTCL), Peter Ngota (wa pili kulia) akijumuika na baadhi ya wateja na
wafanyakazi wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma
kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya
Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi
na viongozi wa kampuni hiyo na wateja kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya
Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho
ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias
Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania
(TTCL), Peter Ngota (kulia) akibadilishana mawazo na mmoja wa wateja wa
kampuni ya TTCL mwenye asili ya China juzi kwenye hafla ya kilele cha
Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la
Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias
Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba ( wa tatu kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya
wafanyakazi na viongozi wa kampuni hiyo na wateja kwenye hafla ya kilele
cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda
la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu
Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI
ya Simu Tanzania (TTCL) imesema itaendelea na utekelezaji wa kuboresha
miundombinu ya mtandao wake wa simu za mezani, mkononi pamoja na huduma
za data ili kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wake na kufikia
kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano nchini. Kauli
hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba alipokuwa akizungumza na
wateja mbalimbali kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma
kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya
Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa huyo wa TTCL, alisema kuwa
maboresho ya miundombinu yanayofanywa kwa sasa katika shirika hilo
yanaliwezesha kukabiliana na changamoto zilizokuwepo awali na kuwapa
wateja weke fursa ya kufurahia huduma mpya na za zamani zinazotolewa
kisasa na kwa umahiri mkubwa hivi sasa.
"Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL) inaendelea na utekelezaji wa uboreshaji wa
miundombinu ya mtandao wa simu za mezani, simu za mkononi na huduma za
Data ili tuweze kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu na kufikia
kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano," alisema
Waziri Kindamba.
Aidha
alifafanua kuwa TTCL inawaahidi wateja wake na taifa kwa ujumla kwamba
itaendelea kutoa huduma bora, za uhakika na gharama nafuu katika
kutengeneza mazingira mazuri ya kiteknolojia, kwani baada ya mabadiliko
watumishi wake wameazimia kuongeza kasi ya kufanya kazi kwa bidii,
uadilifu, ubunifu na uzalendo wa hali ya juu ili kwenda sambamba na
mahitaji ya sasa na baadaye ya wateja wa sekta ya Mawasiliano.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya
TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo
lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki,ya Huduma
kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya
Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Sabasaba jijini Dar es Salaam
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya
TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo
lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma
kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya
Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere,
Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na hayo Kindamba aliwataka wateja hasa taasisi na makampuni mbalimbali
ya nje na ndani ya nchini kukitumia Kituo cha Taifa cha Kutunzia
kumbukumbu (National Internet Data Centre) ambacho Ujenzi wake
umekamilika na kimeanza kufanya kazi hiyo, huku kikiwa cha kisasa na
chenye hadhi ya kimataifa.
"...Niwashukuru
sana wateja ambao wameishakubali kuifadhi taarifa zao kwenye Kituo.
Nafahamu kwamba mazungumzo yanaendelea kati yetu na Wateja wengine na
ninaamini kuwa tutakubalina na kufanya kazi pamoja...natoa wito kwa
Wateja na Wadau wote wa ndani na nje ya nchi, tutumie kituo hiki chenye
ubora wa Kimataifa na hadhi ya juu kabisa hapa nchini na eneo zima za
Afrika Mashariki," alisema Kindamba.
Aliongeza
kuwa kwa sasa kampuni ya TTCL imejipanga vyema kufanya kazi kwa
ufanisi, huku ikitekeleza kwa vitendo falsafa ya Serikali ya awamu ya
tano ya Hapa Kazi Tu. TTCL pia imedhamiria kutumia kwa uaminifu mkubwa
rasilimali zilizopo ili iweze kutoa mchango stahiki katika mageuzi
yanayoendelea ya kuifanya Tanzania kupiga hatua kuelekea kuwa Nchi ya
Uchumi wa Viwanda.
"Lengo
hili la kuifanya Nchi kuwa ya Uchumi wa Viwanda, litafikiwa kwa uhakika
zaidi endapo huduma za Mawasiliano zitakuwa za uhakika. TTCL tupo
tayari na tunao uwezo wa kufanikisha lengo hili pasi na shaka yoyote.
Sote
tunafahamu nia ya dhati ya Serikali yetu ya awamu ya Tano chini ya Rais
wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli. Serikali yetu inataka kazi kwa
vitendo, inataka huduma bora kwa Wananchi," alisisitiza Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL, Kindamba.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Thomas
Mushi (wa pili kulia) akipata picha na baadhi ya wageni waalikwa kwenye
hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika
ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja
vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa pili
kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Edwin Mashasi.
No comments:
Post a Comment