Friday, October 28, 2016

Exim Benki yaboresha huduma kwa wateja wake, wazindua tawi la Temeke jijini Dar.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda amesema kwasasa wamedhamiria kuboresha huduma zao katika maeneo mbalimbali na kuahidi wateja kuendelea kuwapatia huduma bora.

“Benki yetu inaendelea kufanya vizuri na tumejipanga kuendelea kuboresha huduma zetu, mwanzoni tulikuwa sehemu nyingine na wateja wetu walikuwa wakituuliza lini tutahamia sehemu iliyo na nafasi nzuri ya kutoa huduma na sasa tumeipata,” alisema Mponda.
Meneja wa Tawi la Benki Exim Temeke, Subira Augustino akiwakaribisha wageni waalikwa ndani mara baada ya ufunguzi kufanyika wa Tawi la Exim Bank Temeke.
Meneja wa Tawi la Benki Exim Temeke, Subira Augustino akitoa neno la ukaribisho kwa wafanyakazi wa Exim Benki na wateja ambao walialikwa kwa ajili ya kushuhudia hafla ya ufunguzi wa Tawi la Exim Temeke. 
Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda akizungumza kuhusu benki ya Exim na jinsi ambavyo wamejipanga kuboresha huduma.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo Wadogo wa Banki ya Exim, Raul Singh akielezea jinsi Exim Bank ambavyo inazidi kufungua matawi maeneo mengine ili kuwasogezea wateja huduma kwa ukaribu.
Wageni waalikwa wakikata keki. Wa kwanza kushoto (mwenye suti nyeusi) ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda, Mteja wa Benki ya Exim, Abdelsamad Hussein, Afisa Mauzo wa Benki ya Exim Temeke, Rashid Bundara, Mteja wa Benki ya Exim, Saamu Omary, Mteja wa Benki ya Exim, Shukran Ezekiel.Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda akimlisha keki Mteja wa Benki ya Exim, Abdelsamad Hussein.
Meneja wa Tawi la Benki Exim Temeke, Subira Augustino akimlisha keki Mteja wa Benki ya Exim, Saamu Omary.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo Wadogo wa Banki ya Exim, Raul Singh akiwagawia keki baadhi ya wateja wa benki hiyo ambao walijumuika nao pamoja katika uzinduzi wa Tawi la Exim Bank Temeke.
Baadhi ya wateja wa Exim Bank wakitoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wa benki hiyo.
Wafanyakazi wa Exim Bank wakiwa katika picha ya pamoja.

Wafanyakazi wa Exim Bank wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wao waliohudhuria halfa ya ufunguzi wa Tawi la Exim Bank Temeke.

No comments: