Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Watendaji mbali mbali wa Serikali mara alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba alipohudhuria sherehe za Siku ya kilele cha Wazee Duniani zilizofanyika wilaya ya Chake chake katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Pemba
Baadhi ya Wazee waliohudhuria katika sherehe za Kilele cha Siku ya Wazee Duniani zilizofanyika katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
Baadhi ya Wazee kutoka Mikoa ya Pemba waliohudhuria katika sherehe za Kilele cha Siku ya Wazee Duniani zilizofanyika katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wazee alipowasili katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika leo Wilaya ya Chake chake katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Mkoa wa Kusini Pemba
Mwakilishi wa Wazee Bw.Salum Ali Mata akisoma risala ya Wazee katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika lWilaya ya Chake chake katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Mkoa wa Kusini Pemba
Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika Wilaya ya Chake chake katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Mkoa wa Kusini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea risala ya Wazee kutoka kwa Mwakilishi wa Wazee Bw.Salum Ali Mata aliyoisoma katikasherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea taarifa ya Shirika la HELP AGE INTERNATIONAL Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi Amleset Tewodoes mara baada ya kuisoma katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Mouldine Syrus Castico akitoa salam zake kwa Wazee pamoja na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Wazee hao katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Wazee katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wazee Duniani zilizofanyika katika viwanja vya nje Uwanja wa Gombani Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba (kushoto) Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Mouldine Syrus Castico na Bw.Salum Ali Mata mwakilishi wa Wazee (kulia)
Picha na Ikulu
-----------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------
Na Rajabu Mkasaba, Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa
kwa kuthamini michango ya wazee, katika kipindi hiki cha pili cha uongozi wa
Serikali ya Mapinduzi, Awamu ya Saba, Serikali itahakikisha inaongeza kasi
katika kupanga na kutekeleza mipango yenye lengo la kuimarisha ustawi wa wazee.
Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hafla ya Kilele cha maadhimisho ya
Siku ya Wazee Duniani, pamoja na kumpongeza Dk. Shein hafla iliyofanyika huko
Gombani, Wilaya ya Chake, Mkoa wa Kusini Pemba na kuhudhuriwa na viongozi mbali
mbali wakiwemo wazee kutoka maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Pemba.
Katika maelezo yake Dk. Shein alisema
kuwa hivi karibuni aliuita uongozi wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee,
Vijana, Wanawake na Watoto ofisini kwake Ikulu kwa lengo la kuja kumueleza
jinsi Wizara hiyo ilivyojipanga katika kutekeleza Ilani ya CCM ya Uchagauzi
Mkuu wa mwaka 2015-2020, Ibara ya 165 iliyoainisha mambo muhimu ya kufanyiwa
wazee.
Dk. Shein alisema kuwa miongoni mwa mambo
ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatakiwa iyatekeleze kwa ajili ya
wazee ni pamoja na kuhakikisha wazee wanatambulikana na kupatiwa huduma za
matibabu bila ya malipo, kuhakikisha wazee wanapatiwa haki zao za kisheria na
kupatiwa fursa sawa katika ngazi zote.
Mambo mengine ni pamoja na kuwalinda
wazee dhidi ya vitendo vya ukatili vikiwemo mateso na mauaji, kuwawekea
miundombinu na mazingira bora yatakayowawezesha kwenda wanapotaka na kutumia
vyombo vya usafiri wa umma kwa gharama nafuu pamoja na kuweka utaratibu
utakaowawezesha wazee kulipwa pensheni.
Dk. Shein alieleza kuwa kwa kutambua
umuhimu wa wazee katika kujenga misingi imara ya maendeleo hapa nchini Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar mara tu baada
ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964 iliandaa na kutekeleza mipango imara ya kuwatunza, kuwaenzi na
kuwaendeleza wazee.
Alisema kuwa juhudi hizo za Serikali
ambazo zinatekelezwa hadi hivi leo pamoja na utamaduni wa Zanzibar unaohimiza
kuwa na mapenzi na wazee kwa kuwatunza na kuwashirikisha katika mipango ya
maendeleo na kifamilia, zimeifanya Zanzibar kuwa ni miongoni mwa nchi bora
katika bara la Afrika inayotekeleza vyema maisha ya uzeeni.
Dk. Shein alisema kuwa mara tu baada ya
Mapinduzi Matukufu ya 1964, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwajengea wazee
nyumba za makaazi, Unguja na Pemba kwa ajili ya kuwaenzi na kuwatunza pamoja na
kuwapa huduma muhimu bila ya malipo mambo ambayo hadi leo yanaendelezwa.
Pamoja na hayo, alieleza kufarajika kwake
na kuanza kutekeleza kwa ufanisi mkubwa mpango wa kuwapatia pensheni maalum
wazee wote wa Unguja na Pemba waliofikia umri wa miaka 70 bila ya kujali
historia ya kazi walizokuwa wakizifanya huku akieleza azma ya serikali ya
kuongeza fedha hizo.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza
kupokea kwa masikitiko suala la udanganyifu uliofanywa na baadhi ya watendaji
wa kuwaingiza baadhi ya watu waliokuwa hawana sifa, katika orodha za wazee
wanaostahiki kupata malipo.
Kutokana na hilo Dk. Shein aliiagiza
Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto kulishughulikia
tatizo hilo na kuwachukulia hatua watendaji wote walioshindwa kuwajibika na
ambao wamelisababisha tatizo hilo.
Dk. Shein alisisitiza kuwa waliofanya
vitendo hivyo si waadilifu na hawana sifa za kufanya shughuli hizo na kueleza
kuwa watu hao wapo na ni lazima wachukuliwe hatua na wawajibishwe.
Dk. Shein alieleza kuvutiwa na kufurahishwa
na kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya siku ya wazee, ambayo inasema
‘Chukua hatua, dhidi ya unyanyasaji wa wazee” na kusisitiza kuwa kauli mbiu
hiyo inakwenda sambamba na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika mapambano
dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, udhalilishaji watoto na vitendo vyote vya
ukatili katika jamii.
Alieleza kuwa hatua kubwa zimechukuliwa
katika kulishughulikia suala la kiinua mgongo kwa wafanyakazi wa Serikali
waliostaafu na kusema kuwa hivi karibuni mnamo mwezi Marchi kiasi cha Tsh.
Bilioni 16.2 zilitolewa kwa ajili ya kuwalipa watu viinua vyao mgongo na wengi
walifaidika hasa wale waliotaka kwenda Hijja.
Nae
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Modelin
Castiko wamo katika mchakato wa kuwapatia vitambulisho maalum wazee ili viweze
kuwasaidia katika kupata huduma muhimu.
Waziri Castiko alieleza jinsi wazee
walivyofarajika na hatua za Serikali zinazochukuliwa kwa ajili yao katika
kuwasaidia katika maisha yao sambamba na kueleza haja ya kuwatunza na kuwaenzi wazee
na watoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Help Age
International Tanzania Bi Amleset Tewodos alisema kuwa Umoja wa Mataifa mwaka
huu umehakikisha kuwa na kauli mbiu ambayo itaondosha ubaguzi kwa wazee.
Alisema kuwa sherehe hizo zinakuja wakati
mwafaka ambapo Rais D. Shein ameaweka peshenai ambayo ni huduma ya kwanza
kutoklewa katika nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa wazee.
Alielezaa kuwa kutolewa kwa pensheni
jamiii itasaidia kuondoa umasikini na inatekeleza malengo endelevu yaliyowekwa
na Umoja wa Mataifa ambapo nchi zote duniani zimeamua kutekeleza hatua hiyo muhinu
itayohakikisha afya na maisha bora kwa wazee.
Nao Wazee wa Zanzibar katika risala yao
walieleza kuwa masuala ya wazee Zanzibar yalianza kushuhulikiwa kabla ya tamko
la Umoja wa Mataifa kwani hatua za kuwatuza wazee na kuwasaidia ilianza rasmi
mara baada ya Mapiduzi ya 1964 chini ya uongozi wa Marehemu Mzee Abeid Amani
Karume.
Wazee hao walieleza kuwa April 15, 2016
Zanzibar iliweka mfamo mpya wa kuwalipa pensheni jamii wazee, chini ya uongozi wa
Dk. Shein kwani huo ni ukombozi wa kuondosha umasikini kwa wazee kwani pesa
walizozipata wanaendesha miradi yao midogo midogo na kuwasaidia katika maisha yao.
Wazee hao walieleza imani yao kwa Rais Dk.
Shein pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na kuziomba Serikali hizo kuwa wazee wajulikane kuwa ni
kundi tete na hivyo linahitaji kuwekewa mipango thabiti ya kuwaendeleza katika
maisha yao.
No comments:
Post a Comment