Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akishiriki katika shughuli ya uchimbaji wa barabara ya Bureni Iramba-Kwanamburi
Mmea aina ya Mrungi umekutwa na Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule ukiwa umestawi
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akiwahutubia wakazi wa Kata ya Vudee katika mkutano wa hadhara
Wakazi wa Kata ya Vudee wakisikiliza kwa makini maagizo ya serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule
Wananchi wa Kata ya Vudee wakishiriki zoezi la uchimbaji wa barabara
Na Mathias Canal, Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule amejumuika na wananchi wa Kata ya Vudee katika shughuli ya uchimbaji wa barabara ya Bureni Iramba-Kwanamburi iliyopo katika kijiji cha Bureni Iramba.
Dc Staki amejitokeza katika shughuli hiyo ikiwa ni muendelezo wa kujumuika pamoja katika shughuli za maendeleo ya wananchi na kuwahamasisha kujitokeza katika kufanya Kazi za maendeleo ya vijiji vyao na kuwafanya wananchi kuiamini serikali yao chini ya Rais wa serikali ya awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Dc Staki amewataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana na serikali katika kuchochea shughuli za maendeleo kwani muda wa kampeni umemalizika hivyo kwa sasa ni wakati wa kufanya Kazi kwa bidii ili kuimarisha kauli mbiu ya serikali ya Hapa Kazi Tu.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliopata nafasi ya kuzungumza n kuuliza maswali wamempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa namna ambavyo anashiriki shughuli za maendeleo hivyo wamemuahidi kumuunga mkono.
Wananchi wa maeneo hayo wametakiwa kujihusisha na shughuli za maendeleo kwa kulima mazao halali ya biashara ikiwemo kulima tangawizi na kuachana na mazao haramu kama ulimaji wa mirungi.
Mara baada ya mkutano huo wa hadhara Mkuu huyo wa Wilaya aliongozana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo walielekea katika kijiji cha Kisesa kwenye shamba la mkulima Bw Johnson Charles Mshana ambaye anajihusisha na kilimo cha Mirungi ambaye pia alikataa Barabara na nguzo za umeme wa Tanesco zisipite shambani kwake kwa ajili ya kuboresha shughuli za maendeleo katika kata hiyo ya Vudee na maeneo ya jirani.
Mara baada ya kufika katika shamba hilo mkulima huyo hakuwepo jambo lililopelekea kukamatwa kwa binti yake ambaye alikutwa kwenye shamba hilo la Mirungi
No comments:
Post a Comment