Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe akizungumza na viongozi watendaji na Maafisa Tarafa.
Hapo ni mkurugenzi mtendaji akizungumza na viongozi watendaji na Maafisa Tarafa.
Mmoja wa Wenyeviti wa Vijiji akizungumza katika kikao kazi hicho.
Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Abel Noel akitoa ufafanuzi wa misingi ya Utawala bora.
Viongozi watendaji, Maafisa Tarafa waliofika katika kikao kazi cha DC.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe amewataka Maafisa Tarafa, Maafisa Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji na Wenyeviti wa Vijiji kusimamia misingi ya utawala bora katika kutimiza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi. Aliyazungumza hayo katika kikao kazi alichokiitisha siku ijumaa tarehe 28/10/2016.
Mh. Gondwe amewataka viongozi kusimamia rasilimali za umma ikiwemo misitu, ardhi na usimamizi wa suala zima la usafi na mazingira katika maeneo yao. Pia aliwakumbusha kusikiliza kero za wananchi kuanzia ngazi ya chini ikiwa na kushughulikia malalamiko yao kabla ya kufika ngazi ya Wilaya. Wananchi wanatakiwa kusikilizwa matatizo yao, pale ambapo ngazi za chini zimeshindwa basi ngazi ya Wilaya itashughulika kikamilifu.
Mh. Gondwe amewaeleza Maafisa Watendaji na wenyeviti wa Vijiji kwamba kutokana na hali mbaya ya chakula suala la kulima ekari moja ya muhogo kwa kila kaya ni lazima sio jambo la hiari tena. Aidha amepiga marufuku kutumia mazao ya chakula katika kutengenezea pombe kwa sababu hali ya chakula kwa sasa katika Wilaya ya Handeni sio nzuri.” Ni marufuku mazao ya chakula kutumika katika kupikia pombe kwa sababu hatuna chakula cha kutosha” alisema.
Ametoa tahadhari kwa viongozi na Watendaji kuwa makini na taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s)zinapokuja kufanya huduma katika maeneo yetu, kwani taasisi nyingine zinakuwa hazina dhamira njema kwa wananchi kwani zimeonekana kufanya mambo ya kitapeli mfano baadhi yao zimekuwa zikichangisha fedha kwa wananchi bila kufuata utaratibu., ,”Viongozi wote na Maafisa Tarafa pale mnapoona kwenye maeneo yenu kuna taasisi zisizo za kiserikali zimekuja na hamuelewi mienendo yao tafadhali naomba mtoe taarifa mapema ili Uongozi wa Wilaya uweze kushughulikia mapema ” alisema.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Handeni aliwataka Kitengo cha misitu kusaidia kuainisha hifadhi za misitu kwa ngazi ya Serikali kuu, Halmashauri na Vijiji ili wananchi waweze kuyatambua na kwamba watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi waondoke wenyewe kwa hiari yao kabla ya Serikali kuu na Halmashauri ya Wilaya haijawaondoa kwa nguvu.
Alisisitiza
kwamba suala la kulinda maeneo ya hifadhi kama vile misitu, vyanzo vya
maji na maeneo yaliyohifadhiwa sio la hiari Aliwataka halmashauri
kuripoti pindi uharibifu wa maeneo hayo unapofanyika . Aidha Alipiga
marufuku pia watoto chini ya umri wa miaka 18 kuchunga ng’ombe hasa siku
za shule na kuwaripoti watu wanaoharibu miundombinu ya maji.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe alisema kutakua na ratiba ya kupanda miti laki 6 kwa msimu unaokuja wa mvua ambapo kila kaya itatakiwa kupanda miche ya miti kumi (10) ambayo watalazimika kuitunza ili iweze kukua.
Mkurugenzi mtendendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya kwamba atasimamia utekelezaji wa maelekezo yote aliyoyatoa ikiwemo utawala bora utakao husisha usomwaji wa mapato na matumizi katika vijiji vyote , utunzaji miti, hifadhi ya misitu na ulinzi wa miundombinu na vyanzo vya maji.
Alda Sadango
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya Handeni
29/10/2016
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe alisema kutakua na ratiba ya kupanda miti laki 6 kwa msimu unaokuja wa mvua ambapo kila kaya itatakiwa kupanda miche ya miti kumi (10) ambayo watalazimika kuitunza ili iweze kukua.
Mkurugenzi mtendendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya kwamba atasimamia utekelezaji wa maelekezo yote aliyoyatoa ikiwemo utawala bora utakao husisha usomwaji wa mapato na matumizi katika vijiji vyote , utunzaji miti, hifadhi ya misitu na ulinzi wa miundombinu na vyanzo vya maji.
Alda Sadango
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya Handeni
29/10/2016
No comments:
Post a Comment