Monday, October 10, 2016

Uzinduzi wa Dar Restaurant Week ulivyofanyika The Bay Restaurant, Dar es Salaam

Kwa wakazi wa Dar es Salaam kuanzia Oktoba, 8 hadi 15 wanataraji kuwa katika Dar Restaurant Week ambayo itawawezesha wateja wa migahawa 10 ambayo inashiriki maadhimisho hayo kupata chakula kwa bei pungufu tofauti na ilivyozoeleka.

Akizungumza Mwanzilishi wa Dar Restaurant Week, Adam Senkoro alisema lengo ya kuanzisha maadhimisho hayo ni kupata pesa kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kike ambao familia zao hazina uwezo wa kuwalipia fedha za masomo, na wao watatumia fedha ambazo zimepatikana kwa siku ya ufunguzi kwa ajili ya kuwalipa masomo.
Mwanzilishi wa Dar Restaurant Week, Adam Senkoro akizungumza kuhusu Dar Restaurant Week na jinsi ilivyo na faida kwa wakazi wa Dar.

Alisema ni fursa kwa wakazi wa Dar kutembelea katika migahawa ambayo inashiriki ili kupata chakula wanachokipenda kwa bei nafuu kwa siku zote ambazo zimepangwa mpaka maadhamisho hayo yatakapomalizika.

“Tumeandaa Dar Restaurant Week na mapato ambayo yatapatikana yatakwenda kusaidia kulipa ada kwa watoto wa kike, ninachotaka kuwaambia wakazi wa Dar ni kutembelea migahawa ambayo inashiriki ili kupata chakula kwa bei ndogo,” alisema Senkoro.
Wahudhuriaji wa uzinduzi Dar Restaurant Week wakilipa pesa kabla ya kuingia ndani.

Wahudumu wa migahawa mbalimbali ambayo inashiriki Dar Restaurant Week wakitoa huduma kwa watu waliohudhuria uzinduzi wa wiki hiyo.

 Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi wa Dar Restaurant Week. Baadhi ya vyakula vilivyokuwepo wakati wa uzinduzi wa Dar Restaurant Week.

Mwanamuziki Grace Matata akitoa burudani pamoja na bendi yake.No comments: