Wednesday, October 5, 2016

BENKI YA DCB YAZINDUA UTARATIBU MPYA KWA WATEJA WAKE WA KUTOA MAONI KWA KUTUMIA MASHINE YA HAPPY OR NOT.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya DCB imezindua utaratibu mpya kwa wateja wake wa kutoa maoni kwa kutumia mashine ya Happy or not katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Ubunifu- DCB, Samwel Dyamo amesema kuwa huduma hii mpya itasaidia kupata taarifa kwa mapema zaidi kwani zitakuwa ni kwa njia ya mtandao na zitatoa mrejesho kwa kampuni ili kuzidi kuboresha zaidi.

Dyamo amesema, kwa sasa wateja wetu watatumia mashine hiyi badala ya kutumia boksi la maoni kwani ni njia rahisi sana kuweza kuwafikia wao kwa mapema kwanj mrejesho utakuja haraka zaidi na mapema.

Kwa pamoja benki ya DCB waliweza kukata keki na kusherehekea na wateja wao huku baadhi wakisifia huduma nzuri zinazotolewa na wanapata mikopo kwa njia rahisi sana na kwa riba nafuu.

Fatma Simba, amesifia huduma za benki ya DCB na kusema kuwa wanatoa mikopo kwa urahisi sana ndani ya siku tatu kuanzia kima cha 50,000.

Wiki ya huduma kwa mteja inaadhimishwa dunia nzima kwa makampuni mbalimbali na taasisi, ambapo Benki ya DCB wamekuja na kauli mbiu ya Wewe ni mhimili wetu, tupo kwa ajili yako. 
 Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Ubunifu DCB, Samwel Dyamo akizindua kwa kubonyeza kutufe katika mashine ya Happy or Not jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo.       
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mind Source, Abubakar Faraji akielezea namna ya kuitumia mashine ya Happy or Not kwa wateja wa Benki ya DCB leo Jijini Dar es salaam kwenye wiki ya Huduma kwa Mteja.
 Wateja na wafanyakazi wa DCB Benki wakiwa wanashuhudia kukata kwa keki sambamba na wateja hao kukata keki.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Mikakati na Uhakiki wa beki ya DCB, Samwel Dyamo akizungumza na wateja wao katika wiki ya Huduma kwa Mteja leo Jijini Dar es salaam.  
 Wafanyakazi wa Benki ya DCB wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Kitengo cha Mikakati na Ubunifu Samwel Dyamo katika maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Mteja tawi la Magomeni. 
Tawi la Benjamin mkapa wakisheherekea wiki ya huduma kwa wateja pamoja na wateja wao. Sambamba  Meneja wa tawi hilo Badru Lashku.

No comments: