Thursday, September 8, 2016

ZANTEL WATOA MBUZI 100 KWAAJILI YA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA VILIVYO CHINI YA BAKWATA JIJINI DAR ES LEO.


Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akikabidhi Mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzani, Sheihk Ally Ngeruko Mbuzi 100 kwajiili ya vituo vya  kulelea watoto yatima vilivyo chini ya BAKWATA vya jijini Dar es Salaam.

 Msaada huo umekabidhiwa kwaajili ya sikukuu ya Kuchinja ya Idd el –Adha ambayo ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza mara baada ya kukabidhi Mbuzi kwa mwakilishi wa Mufti wa Tanzania ili aweze kugawa kwenye vituo vilivyo chini ya BAKWATA katika mikoa ya hapa nchini.

Amesema Zantel wameona sikukuu hiyo ya Idd el –Adha ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha kwa kuonyesha umuhimu wa kutoa sadaka kwa kuchinja na ibada.

Mbuzi 400 watatolewa kwa wateja wa Zantel wenye matumizi zaidi kuliko wengine na ambao watakuwa wamejisajili katika kampeni kwa kupitia *149*15# na kuchagua  “Jibwage na Mbuzi”. Kujisajili katika promosheni hii ni bure kwa wateja wote wa Zantel. Kila siku wateja 40 watakaokuwa wametumia muda zaidi watajizawadia mbuzi.

“Hii si bahati nasibu, wale wateja wa juu watakaokuwa wametumia dakika nyingi bila kuchezeshwa mchezo wa bahati watakuwa wamejizawadia moja kwa moja hivyo natumia fursa hii kuwahamasisha wateja wetu kujisajili ili kupata mbuzi na kusambaza furaha ya Eid katika familia zao” amesema  Benoit.
Baadhi ya Mbuzi zilizotolewa katika Baraza la Kiislam Tanzania (BAKWATA) ambazo ni kwaajili ya Vituo vya kulelea watoto yatima  vya Mikoa ya hapa nchini ikiwa ni moja ya sikukuu ya Idd el –Adha ni moja ya sikukuu mbili muhimu za Kiislamu ambayo waumini wa dini ya kiislamu huiadhimisha.
Mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zuberi, Sheihk Ally Ngeruko akiwashukuru Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi Zantel  kwa kutoa mchango wao katika Baraza la Kiislamu Tanzania (BAKWATA) amewaombea Mungu awaongezee walipotoa kwaajili ya watoto wa Kituo hicho.
Baadhi ya walezi wa Kituo hicho na wafanyakazi Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Zantel wakiwa katika shule ya Kiislamu ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya Picha za Makabidhiano.

No comments: