Chacha Masinde kutoka mkoani Mara akimaliza Rock City Marathon na kuwa
mshindi wa kwanza kwenye mbio hizo zilizofanyika Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza jana . Chacha alitumia muda wa saa 01:03:00 kumaliza mbio
hizo akifuatiwa na mshiriki kutoka nchini Kenya David Kilimo aliyetumia
muda wa saa 01:04:40.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw John Mongella sambamba na
maofisa kutoka benki ya NMB wakishiriki mbio
za za km 5.
Washiriki wa mbio za km
21 wakiondoka Uwanja
wa CCM Kirumba kuanza safari ndefu.
Ushindani
ulikuwa ni mkubwa!
Washiriki
kutoka pande tofauti za Dunia washiriki.
Ilikuwa
ni furaha tupu kwa washiriki
Watoto
nao hawakuwa nyuma…mbio zilihusisha watu kutoka rika zote kwa kuzingatia vigezo
na mashariti.
Suala
la usalama kwa washiriki ilikuwa miongoni mwa agenda za msingi kwenye mbio
hizo.
Watu
wenye ulemavu wa ngozi walishiriki mbio za km 5.
Mwandishi wetu, Mwanza
Chacha Masinde kutoka mkoani
Mara ameibuka mshindi wa kwanza kwenye mbio za Rock City
Marathon zilizofanyika jana jijini Mwanza baada ya kumaliza kwa muda wa saa
01:03:00, akifuatiwa na mshiriki kutoka nchini Kenya David Kilimo aliyetumia
muda wa saa 01:04:40
Mbio hizo za kilomita 21
zilianzia Uwanja wa CCM Kirumba kupitia Barabara ya ikulu ndogo hadi
mzunguko wa samaki na kuelekea Buzuruga kisha kutokea barabara ya
pasiansi na kumalizikia uwanjani Kirumba huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John
Mongella akishiriki kukimbia mbio za km 5 sambamba na watu wenye ulemavu wa
ngozi yaani Albino.
Nafasi ya tatu upande wa wanaume
ilichukuliwa na Mkenya Moris Mosima aliyetumia muda wa saa 01:04:57,
ikiwa sekunde chache nyuma ya mpinzani wake.
Akizungumzia siri ya ushindi wake,
Chacha siri ya mafanikio hayo ni kujituma kwake zaidi katika kufanya mazoezi
maalum kwa ajili ya mashindano hayo ili kuhakikisha kwamba mwaka huu mshindi wa
kwanza katika mbio hizo anatoka nchini Tanzania tofauti na miaka ya nyuma
ambapo washindi walikuwa wakitoka nchini Kenya.
“Niliweka nadhiri nikasema mwaka huu lazima
mshindi atoke Tanzania zaidi niwe mimi na ninashukuru nimetimiza adhama yangu.
Pamoja na hilo maandalizi ya mwaka huu yamekuwa mazuri zaidi mahitaji yote
muhimu yakiwemo maji tukiwa njiani yamesaidia mafanakinio hayo licha ya
washiriki kuwa zaidi mwaka huu hatua ambayo iliongeza changamoto kwetu zaidi,’’
alisema.
Upande wa wanawake
mshindi wa kwanza ni Mtanzania pia Faimina Abdi kutoka mkoani Arusha
aliyetumia muda wa saa 01:13:12 akifuatiwa na mwenzake kutoka
mkoani Arusha Angelina Daniel aliyetumia saa 01:14:38 huku Mkenya Dorifine
Omary akishika nafasi ya tatu akitumia saa 01:16:54
Washindi wa kwanza
katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya nane jijini Mwanza waliibuka
na kitita cha Sh1.5 milioni kila mmoja, washindi wa pili Sh900,000 na
washindi watatu Sh700,000.
Mashindano hayo ya kila mwaka
yaliyokatika kalenda ya RT yaliandaliwa na Kampuni ya Capital Plus kwa udhamini kampuni za Freidkin Conservation Fund na African
Wildlife Trust, Benki ya NMB, New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma
Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door.
Akizungumza kabla ya kukabidhi
zawadi kwa washindi kwa washindi na washiriki wa wa mbio hizo Mkuu wa
mkoa wa Mwanza, Bw John Mongella ambae pia alishiriki mbio hizo kwa kukimbia
mbio za km 5 alisema mbio hizo ni nyenzo muhimu ya kuwaandaa wanariadha nchini
kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa na
kuirudishia nchi heshima yake katika mchezo huo.
“Ndio maana tumekuwa
tukisisitiza wadhamini waendelee kujitokeza kusaidia mbio hizi ili ziendelee
kuwa bora zaidi,’’ aliongeza.
Akikabidhi zawadi kwa washindi wa mbio
hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba kwa niaba ya Katibu tawala jana,
Afisa michezo mkoa waMwanza James William alisema mbio hizo ni nyenzo
muhimu ya kuwaandaa wanariadha wetu nchini kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri
katika michuano ya kimataifa na kuirudishia nchi yetu heshima ya kipekee katika
mchezo huo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Alisema: “Tanzania inaweza
kurejea katika ramani ya dunia kwenye michezo kama tukijikita katika maandalizi
mazuri ya kuibua na kuviendeleza vipaji vya vijana wetu nchini hasa kuanzia
ngazi ya shule za msingi.”
Naye Mbunge wa jimbo la Ilemema
ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Ntumba na Maendeleo ya Makazi Bi
Angelina Mabula alipongeza waandaaji wambio hizo na kutoa wito kwa washiriki
walioshindwa kufanya vizuri kwenye mbio hizo kutokata tama bali wajiandae na
mashindano yajayo ili waweze kufanya vizuri.
Naye Makamu Mwenyekiti wa mbio
hizo Bw Zenno Ngowi alisema mbio hizo zimeweza kufanyika kwa mafaniko makubwa
na ushirikiano walioupata kutoka uongozi wa mkoa wa Mwanza na mikoa jirani huku
pongezi pia zikielekezwa kwa jeshi la
polisi kwa kuhakikisha kila kitu kinaisha kwa usalama
No comments:
Post a Comment