WAHITIMU waliosoma Shule ya Sekondari Kilakala , iliyopo mkoani Morogoro wameombwa kujitokeza kuunga mkono mpango wa Serikali wa uimalishaji wa miundombinu ya elimu itakayoweka mazingira mazuri yatakayowavutia wanafunzi kusoma.
Rai hiyo imetolewa na wahitimu wa mwaka wa masomo 1986 hadi 1995 ambao wameanzisha umoja wao ukiwa na lengo la kusidia utatuzi wa changamoto mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa huduma za afya kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Muhitimu wa zamani wa shule hiyo , Wanyenda Kuta , aliyeambatana na wenzake 15 waliosoma kwenye hiyo ya wasichana wenye vipaji maalumu , Augosti 27, mwaka huu alisema, shule ya Kilakala imetoa wahitimu wengi wanawake.
Alisema , asilimia kubwa ya waliohitimu katika shule hiyo ni watumishi katika ngazi mbalimbali za Kiserikali , Viongozi wa kisiasa , Mashirika ya Umma , Sekta binafsi na wajasilimali wakubwa .
Hivyo alisema , wao walipita katika mikono salama ya shule, walimu ,wazazi na Serikali na kwa sasa wanao wajibu wa kurudisha kidogo wanachokipata kwa kusaidiana na Serikali kwenye mpango yake ya kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo katika shule hiyo.
“ Kufika kwetu hapa kumetokana na wananchi kulipa kodi za Serikali ambayo ilijenga shule hii ambayo imetuwezesha sisi kupata elimu bora hapa Kilakala” alisema Kuta.
Hivyo alisema , kwa kutambua umuhimu huyo, wahitimu hao waliamua kuchangishana fedha na kupatikana kiasi cha Sh milioni tatu zilizosaidia kununua shuka, magodoro na ukarabati wa Zahanati ya Shule ili hiyo.
Pamoja na hayo ,alitumia nafasi hiyo kuwasihi wanafunzi wakike wanaosoma katika shule hiyo wajitambue kuwa wanaowajibu nao kuja kulisaidia taifa lao kwa vile Serikali inatumia kodi za wananchi katika kuboresha mazingira ya elimu nchini.
“ Kilakala Sekondari imetoa na itaendelea kutoa wataalamu wa fani mbalimbali nchini , na wale ambao ni matunda ya shule hii tuangalie tulikotoka “ alisema Kuta na kuongeza kuwa.
“ Jambo ambalo tunaweza kulifanya ni kuchangia kuboresha shule yetu ikiwezekana kuanzisha siku maalumu kwa wote waliosoma hapa ili michango yetu isaidia kuboresha shule hii , tunao baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini wakiwemo mawaziri ” alisema Kuta.
Kwa upande wake Kiranja mkuu wa shule hiyo, Gema Kataraiya, pamoja na Kiranja wa Afya kwa nyakati tofauti waliwapongeza wahitimu hao kwa kutoa mashuka na kukarabati jengo la Zahanati ya shule hiyo'
Pamoja na ukarabati wa Zahanati hiyo, wanafunzi hao walisema bado kuna upungufu mkbwa wa vifaa vya kutolea huduma vikiwemo vipimo vya malaria na mazingira yasiyo rafiki ya vyoo.
Awali, Makamu Mkuu wa Shule hiyo upande wa Taaluma, Mussa Katunzi, alisema kuwa mchango uliotolewa na wahitimu hao ni moja ya chachu ya kuwavuta wengine aliosoma shule hiyo kuona nao wanaowajibu wa kuchangia maendeleo ya elimu .
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda umoja wao wakiimba wimbo wa shule ikiwa ni ishara ya kukumbuka walipokuwa wanafunzi shuleni hapo baada ya kufika shuleni hapo Augosti 27, mwaka huu kukabidhi msaada shuka na madogoro kwa ajili ya Zahanati ya shule ambayo pia ilikarabatiwa na michango yao.
.............................. .
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda umoja wao wakiekelea jengo la Ofisi ya Mkuu wa shule kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni.
Mhitimu wa shule ya Sekondari Kilakala , Claudia Iringo akimkaabidhi mwanafunzi wa shule hiyo madafyari kwa ajili ya wenzao wenye mahitaji maalumu , wahitimu hao wa zamani wapatao 15 waliosoma kuanzia 1988 hadi 1995 waliitembele shule yao Augosti 27, mwaka huu .
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda umoja wao wakiwa katika Ofisi ya Mkuu wa shule kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni wa shule baada ya kufika shuleni hapo Augosti 27, mwaka huu kukabidhi msaada shuka na madogoro kwa ajili ya Zahanati ya shule ambayo pia ilikarabatiwa na michango yao.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala,inayomilikiwa na Serikali wakifurahia kuona wahitimu wa zamani katika shule hiyo wamewakumbuka kwa kutoa kmsaada shuka na madogoro kwa ajili ya Zahanati ya shule na kulikarabati jengo hilo.
Picha ya pamojana mwalimu na viongozi wa wanagfunzi
Wahitimu wakiangalia shughuli za shule yao
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda umoja wao wakiimb na kicheza kukumbusha enzi zao katika shule hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa mwaka 1986 hadi 1995 wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kilakala , inayomilikiwa na Serikali ambao wameunda umoja wao pamoja na baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa shule hiyo, walimu na bodi ya shule wakiwa ndani ya jengo la zahanati ya shule baada ya kukabidhi shuka, magodoro pamoja na madatfari kwa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment