Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina
akipanda mti katika Shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete, Jijini Dar es
Salaam leo ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya upanadaji miti Jijini Dar es Salaam iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul
Makonda, Kampeni hiyo ijulikanayo kama "Mti Wangu" itazinduliwa kesho
Oktoba Mosi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan. Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania umechangia miche ya miti 600 katika shule hiyo na miche ya miti
mingine 3,000 itatolewa kesho wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa
ajili ya Jijiji la Dar es Slaam, katika awamu ya pili watachangia tena
miche ya miti 5,000.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina
(wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mama Salma Kikwete,
Elestina Chanafi (wa pili kushoto) baadhi ya miche ya miti kati ya miche 600 iliyotolewa na Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya shule hiyo kuunga mkono Kampeni ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya upandaji wa miti Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos
Santos Silayo (kulia) akimkabidhi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa pili kulia) miche 600 ya miti iliyotolewa na ofisi yake kwa ajili
ya shule ya Sekondani ya Mama Salma Kikwete Jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni hatua
ya kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya upandaji wa miti Jijini Dar es Salaam ijulikanyo
kama “Mti Wangu” . Katika uzinduzi huo
TFS imechangia miche ya miti 3,000 kati ya miche 8,000 ambayo imepanga kutoa
kwa ajili ya kupandwa katika Jiji la Dar es Salaam.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos
Santos Silayo akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Msanii
wa Filamu nchini, Jackline Wolper (katikati) akizungumza na waandishi
wa habari katika hafla hiyo kuhusu kampeni yake ya "Think Green" katika
kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ijulikanayo kama "Mti Wangu" ambayo itazinduliwa kesho Oktoba Mosi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan . Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos
Santos Silayo (kushoto) akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari
ya Mama Salma Kikwete Jijini Dar es Salaam leo katika hafla fupi ya
upandaji wa miti shuleni hapo kuunga mkono Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam ya upandaji wa miti, Prof. Silayo amewaasa wanafunzi hao
kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti.
Katika hafla hiyo TFS wamekabidhi jumla ya miche ya miti 600.
Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Luhaga Mpina (wa tano kushoto), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (wa sita kushoto), Msanii Jackline Wolper, Watumishi na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mama Salma Kikwete.
(Picha na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)
No comments:
Post a Comment