Mwenyekiti wa wadau wa barabara Tanzania Eng. Abdul Awadhi (Kushoto) akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng .Joseph Nyamhanga (Kulia) wakati wa mkutano wa Saba wa wadau wa miundombinu ya reli na barabara,jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa wadau wa barabara Tanzania Eng. Abdul Awadhi akiongea na wadau wa miundombinu ya barabara na reli wakati wa mkutano wa Saba wa wadau hao, uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wadau wa miundombinu ya barabara na reli wakati wa mkutano wa Saba wa wadau hao, uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Wa pili kutoka kulia) akijadiliana na wadau wa miundombinu ya barabara na reli mara baada ya kufungua mkutano huo.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Eng .Joseph Nyamhanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua ramani inayonyesha miundombinu ya barabara nchini wakati wa uzinduzi wa mkutano wa saba wa sekta ya Miundombinu ya barabara na reli, jijini Dar es salaam.
Picha na Benjamin Sawe-Maelezo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa sekta ya miundombinu ya Reli na Barabara kushirikiana na Serikali katika kuchangamkia fursa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta hiyo hapa nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Saba wa wadau wa Sekta hiyo, Prof. Mbarawa amesema kwa sasa Serikali kupitia Rais wa Awamu ya Tano inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Tanga hadi nchini Uganda, ujenzi wa barabara ya kulipia wa Dar es Salaam-Chalinze KM 144 (Dar-Chalinze Express way) na ujenzi wa reli ya kati hivyo ni muhimu kwa wadau hao kutumia mkutano huo katika kuijadili miradi hiyo.
“Ni matumaini yangu katika mkutano huu mtajadili kwa pamoja namna ya kushirikiana na Serikali katika kutekeleza fursa za ujenzi wa miundombinu hapa nchini ikiwemo kuungana na Serikali (Public Private Partnership) au kwa njia nyingine yoyote”, amesema Waziri Mbarawa.
Amesisitiza wadau hao kuja kwa wingi nchini na kuwekeza katika sekta hiyo ili kupanua ushindani wa kibiashara katika soko la kitaifa na kimataifa.
Waziri Mbarawa amebainisha kuwa Serikali inaendelea kutafuta pesa kutoka kwa wadau mbalimbali na kushirikisha taasisi binafsi kupitia mpango wa kushirikiana baina ya Serikali na Taasisi hizo (Public Private Partnership) ili kutekeleza miradi ya miundombinu ya reli na barabara nchini.
Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Eng. Bruno Ching’andu amesema kuwa licha ya TAZARA kuwa na treni za umma zinazotoa huduma za usafiri nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa fedha katika uendeshaji wa shirika hilo ikiwemo gharama za ujenzi na ukararabati wa mabehewa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment