Wastaafu wa Jeshi la Magereza wakiwasili katika Viwanja vya Chuo
cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga, Dar es Salaam wakiwa
wameongozwa na Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile
wakielekea Jukwaa Kuu kupokea Salaam ya Heshima. Hafla ya kuwaaga
wastaafu wa Jeshi la Magereza imefanyika leo Septemba 23, 2016.
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akiwa katika
Jukwaa Kuu akipokea Salaam ya Heshima kutoka kwenye Gwaride Maalum
la kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza.
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akikagua
Gwaride Maalum la kuwaaga Wastafu wa Jeshi la Magereza lililoandaliwa
na Maofisa wa Jeshi la Magereza.
Gwaride M aalum likipita mbele ya Jukwaa kwa Heshima.
Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakipiga Saluti wakati
Gwaride Maalum likipita mbele ya Jukwaa kwa heshima. Wa kwanza kulia
ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akiwa pamoja
na Wastaafu wengine wa Jeshi la Magereza wakitoa Salaam za mwisho
wakiwa kwenye magari wakati Gwaride Maalum likiwa limeunda Umbo la
OMEGA.
Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakipunga mikono ikiwa ni
ishara ya kuwaaga Wastaafu hao wakati wakipita katika magari Maalum
(hawapo pichani).
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile akipita
kwenye gari Maalum akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuwaaga
Watumishi wa Jeshi la Magereza baada ya kustaafu rasmi Utumishi wa
Umma kwa mujibu wa Sheria.
Kamishna Mstaafu wa Magereza Deonice Chamulesile(katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Wastaafu wa Jeshi la Magereza pamoja
na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(wa pili kushoto) ni Kamishna
wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(Picha zote na
Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment