Friday, September 9, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Waziri wa afya, Ummy Mwalimu awasilisha mswada wa sheria ya mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali wa mwaka 2016 na mswaada wa sheria ya uanzishwaji wa baraza la wanataaluma wa kemia wa 2016 bungeni hii leo. https://youtu.be/BETOqbLyufA
Rais John Magufuli ameteua matakatibu tawala wawili wa mkoa wa Mara na Rukwa kutokana na makatibu tawala wa mikoa hiyo kustaafu. https://youtu.be/lJyXnUnWVC8
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma amesema hatosita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaopinga utekelezaji wa mpango wa matumizi bora ya ardhi unaotekelezwa na serikali  unaolenga kuondoa migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji. https://youtu.be/QFTIRQweeTY
Wadau wa mafao ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini waiomba serikali kuurejesha kwa wadau mswada wa mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii unaolenga kuondoa fao la kujitoa. https://youtu.be/7BdiFlHwvm8
Mkuu wa mkoa wa Tabora atoa rai kwa wakazi wa mikoa ya Kigoma, Singida na Katavi kutumia fursa za kibiashara mara ujenzi wa reli ya kisasa utakapo kamilika ili waweze kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi. https://youtu.be/e7rQwaZswuU
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, yatoa tahadhali kwa watoa huduma za mawasiliano na wateja wake kujihadhari na matapeli kupitia mitandao. https://youtu.be/OZ5f11_M33g
Taasisi ya sekta binafsi nchini TPSF yaandaa kampeni maalumu ijulikanayo kama ‘FAHARI YA TANZANIA’ itakayo hamasisha uzalishaji wa bidhaa katika viwango vilivyo bora.https://youtu.be/xP1Cx0tLoX0
Msafara wa makamu wa rais Mama Samia Suluhu Hassan umepata ajali baada baada ya gari moja kuacha njia na kupinduka. https://youtu.be/GsMB2Nbdo1w
Baadhi ya wadau wameanza kujitokeza kuisadia hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam baada ya kuripotiwa kuwa na uhaba wa vifaa katika hospitali hiyo.https://youtu.be/J1nWhA09QOM
Rais Dr John Pombe Magufuli ateua matakatibu tawala wawili wa mkoa wa Mara na Rukwa kutokana na makatibu tawala wa mikoa hiyo kustaafu. https://youtu.be/jCfLHZ-ueyU
Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Kaliua mkoani Tabora wanaotakiwa kuhama wamemuomba rais kuwasaidia kutokana na kutokuwa na pa kwenda.https://youtu.be/B2zIy5dKbg4
Watu watatu walipoteza fahamu hapo jana baada ya nyumba waliokuwa wakihifadhi fedha zao za vikoba kuteketea kwa moto. https://youtu.be/B2XJ3ahJ5Os
Kambi ya upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi imeendelea kupata ufadhili kutoka kwa wadu mbalimbali. https://youtu.be/234_M_j7kP8
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari DSJ wametembele kituo cha televisheni cha Chanel ten ili kujifunza masuala mbalimbali. https://youtu.be/MskpPEM90qg
Wafanyabiashara wa visima vya mafuta katika mkoa wa Mbeya wameiomba serikali kuwanunulia mashine za EFD kutokana na mashine hizo kuuzwa kwa bei ya juu.https://youtu.be/BMIuHG0YNKk
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imezindua hudua ya Wekesha inayohusu mteja kulipia simu ya kisasa ya mkononi kidogo kidogo. https://youtu.be/AhQXK1H086Y
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu amekitaka kiwanda cha kusindika na kukamua alizeti mkoani Manyara kutoa fursa za ajira kwa vijana mkoani humo.https://youtu.be/8a1yBHVtr8U
Kocha na mchezaji mahiri wa zamani wa taifa Stars Mohamedi Msomali amezikwa leo huko mkoani Morogoro. https://youtu.be/jU80o8Mx-d4
Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea tena kesho kwa michezo tofauti huku Yanga wakiikaribisha Majimaji ya mjini Songea. https://youtu.be/vCYyrk3PRF4
Mwanariadha wa Ethiopia na mshindi wa medali katika michuano ya Olympic aliyeshangilia kwa kuonesha alama ya kuipinga serikali ya Ethiopia amewasili nchini Marekani. https://youtu.be/aZw7WRrrc-U
Ligi kuu Tanzania bara inatarajiwa kuendelea tena hapo kesho wakati Yanga inatarajiwa kuikaribisha Majimaji ya mjini Songea. https://youtu.be/UVD7XClb2yc
Timu ya soka ya wanawake ya taifa Kilimanjaro Queens imeagwa leo kwenda nchini Uganda kushiriki mashindano ya Challenge. https://youtu.be/wMIyN6aLhLo
Mazishi ya aliyekua kocha wa timu ya taifa na mchezaji wa timu ya Yanga Mohamedi Msomali yamefanyika leo katika manispaa ya Morogoro. https://youtu.be/NpZw7iP4F-w
Kivumbi cha ligi kuu ya Uingereza kinatarajia kuikutanisha miamba miwili kesho timu ya Manchester United dhidi ya Manchester City. https://youtu.be/oP0bHuBBxHE

No comments: