Tuesday, September 6, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Wakazi wa kijiji cha Kaskazi katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida, wamekaidi agizo la serikali linalowataka kuhama maeneo ya hifadhi wakitaka kulipwa fidia kwanza;https://youtu.be/JAI2BaDaT3E

SIMU.TV: Baraza la mitihani la taifa NECTA, limeziagiza kamati za mitihani mikoani kote kuhakikisha taratibu za mitihani ya taifa zinazingatiwa ipasavyo;https://youtu.be/4yu3CYLYaNA

SIMU.TV: Ruzuku ya fedha zinazotolewa na serikali kupitia TASAF, zimepunguza tatizo la utoro kwa wanafunzi wilayani Misungwi mkoani Mwanza; https://youtu.be/t_EiQuvRpHA

SIMU.TV: Rais wa Sudan kusini Salva Kiir na Pierre Nkurunzinza wa Burundi wamemtumia ujumbe Dr Magufuli kuwa hali ya usalama katika nchi zao imetengemaa;https://youtu.be/3FVKd6yicDY

SIMU.TV: Serikali imesema itahakikisha wananchi wanapata habari bila kuwepo na kikwazo chochote kitakachosababisha kukosekana kwa upatikanaji wa habari;https://youtu.be/z1JxAUOmCIg

SIMU.TV: Makamu wa rais Samia Suluhu, amesema serikali itaendelea kutengeneza miundombinu mbalimbali ili kuweza kuvutia wawekezaji sekta ya utalii;https://youtu.be/IWVY_mZCrro

SIMU.TV: Meneja msaidizi wa benki kuun kitengo cha uchumi Evarist Mgangaluma, amesema watanzania wanatakiwa kuongeza kiwango cha uzalishaji ili kukuza soko letu la bidhaa nchini; https://youtu.be/n__Y-01ihSY

SIMU.TV: Benki ya FNB imeendesha droo yake ya mwisho ya kampeni ya kuhimiza watanzania kujiwekea akiba huku watanzania mbalimbali wakishindia mamilioni ya fedha;https://youtu.be/gC2dCRZ0XtE

SIMU.TV: Benki ya NMB mkoani Mtwara imetoa mafunzo kwa wafanyabiashara mbalimbali mkoani humo kuhusiana na jinsi ya kuendesha biashara zao na masuala ya bima; https://youtu.be/y52MnNJ4kl4

SIMU.TV: Kocha mkuu wa taifa stars Charles Boniface Mkwasa, amedokeza kuwa anaweza kuacha kuinoa timu hiyo mara tu mkataba wake utakapomalizika hapo March mwakani;https://youtu.be/H1VeDXwF_QQ  

SIMU.TV: Nyota wa zamani ligi kuu ya Uingereza Paul Scholes amesema ligi kuu ya Uingereza kwa sasa haina wachezaji hodari na kushauri kwamba panahitajika marekebisho kadhaa kuboresha ligi hiyo; https://youtu.be/jnuckEWnQQ8

SIMU.TV: Nahodha wa Uingereza Wayne Rooney, ameambiwa kuwa alistahili kuacha kuichezea timu hiyo kwa sababu hana msaada tena kwa timu pia alipaswa kuachana nayo baada ya kumalizika kwa Euro; https://youtu.be/qdYfDv41AU8

No comments: