Tuesday, September 20, 2016

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE WANAODAI SERIKALI WALIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA WANALIPWA FEDHA ZAO

 MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiongea na
walimu wote wa
shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha  ,waratibu elimu,wakaguzi
elimu pamoja na maafisa elimu kata
 Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiwa anaongea na walimu waliouthuria mkutano huo


Habari picha na Woinde Shizza,Arusha


MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la
Arusha Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai  walimu ya
milioni 154  ndani ya wiki mbili  ambayo wamekuwa wakidai  serikali
kuu kwa  muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao
kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi.
Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa
shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha  ,waratibu elimu,wakaguzi
elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto
zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi.
Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na
kwamba  hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya
likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu
ndio inayopaswa  izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo
linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufudisha na kufuatilia kila
siku madeni hayo.
  “mkurugenzi nakupa muda wa wiki mbili deni hili la milioni 154 kwa
ajili ya walimu akikisha zinalipwa haraka iwezekanavyo wakishalipwa
ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa kwani
haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku
wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo
hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa fedha hizo ambazo ni
madeni hayo  zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba atahakikisha
kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani za
halamshauri hiyo  ili zikija zirejeshwe.
Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka kwenye fedha alizoziokoa
ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa madiwani  ambapo
kiasi cha milioni   130  zilizokuwa zinatumika  kuwalipia madiwani
mafuta ,simu   pamoja na nauli zitaelekezwa kulipa walimu hao madai
yao  ili waweze kujikimu na hali wanayokabiliana nayo.

‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya mafuta ni milioni 40.8,fedha
za simu za madiwani milioni 61.2,nauli iliyookolewa milioni 28 ambapo
jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume hivyo fedha hizi
zinaelekezwa kwa walimu wa msingi na sekondari ikiwa ni madeni
wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lkni
tumeona tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha
watoto wetu vizuri”alisema Kihamia .
Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha hizo kwa walimu hao wakati
wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili waendelee kujikimu
kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea hivyo
zitaongeza  ufanisi  kwa walimu  katika kufundisha wanafunzi na akili
zao  na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili wapate elimu
bora.
Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao walisema kuwa wanakabiliwa na
tatizo la kutopandishwa madaraja kwa  waliokaa kazini muda mrefu  huku
wengine walioingia kazini muda mfupi  wakiwa wanapandishwa madaraja
bila kujua vigezo  hivvyo  kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.






 wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthumani Kihamia akiwa anasikiliza kwa makini malalamiko ya walimu hao


 picha ya juu na chini ni walimu waliouthuria mkutano huo wa mkuu wa mkoa  uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC uliopo mkoani Arusha

No comments: