Washindi
wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya sauti waliopatikana katika
shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za
makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China wakionesha tuzo
baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Anastazia Wambura katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo.
Washiriki 10 walishinda mashindano hayo. Kutoka kushoto ni Hilda
Malecela, Safiya Ahmed na Sadiq Kututwa.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura
akisalimiana na mmoja wa washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti,
Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya
StarTimes jijini Beijing, China wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya
Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akizungumza na washindi hao.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,. Anastazia Wambura
akiwasisitizia jambo mshindi wa kwanza hadi wa tatu baada ya kuwakabidhi
tuzo zao.
Washindi
10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao
watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China
wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka (kushoto) Muwakilishi wa
Mamlaka ya Halmashauri ya Beijing, Yang Peili, Meneja Mkuu wa Shirika
la Utangazaji la Taifa, Dk. Ayoub Riyoba, Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Muwakilishi wa Ubalozi
wa China nchini, Guo HaoDong, Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,
Guo ZiQi na Kansela wa Utamaduni katika Ubalozi wa China nchini
Tanzania, Gao Wei wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya
Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
Washindi hao 10 wakifurahia baada ya kukabidhiwa tuzo.
Na Dotto Mwaibale
STARTIMES
imefanya Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na Filamu za
Beijing ya mwaka 2016 kwa mara ya pili jijini Dar es Salaam kwa lengo
lakuendelea kukuza ushirikiano wa iutamaduni baina ya China na Tanzania.
Akizungumza
wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency
Kilimanjaro jijini Dar es Salaam leo asubuhi, mgeni rasmi Naibu Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa
kwa muda mrefu serikali ya China na Tanzania zimekuwa na mahusiano
mazuri katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
“Mahusiano
mazuri ya kiutamaduni ndiyo yaliyopelekea serikali hizi mbili kuendelea
kushirikiana na kuwa marafiki mpaka hivi leo. Uhusiano huo si tu
unatunufaisha katika masuala ya kiuchumi bali pia kijamii.
Kupitia
kazi za sanaa kam vile tamthiliya za michezo ya kuigiza na filamu watu
huweza kujua na kujifunza tamaduni za kila upande.
Nawapongeza
StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China nchini Tanzania kwa
kutuletea maonyesho haya ambayo nina hakika yatakuwa na manufaa makubwa
kwa tasnia yetu.” Alisema . Wambura
“Pia
ningependa kuwapongeza StarTimes kwa juhudi zao za dhati katika kukuza
utamaduni wetu kuipa nafasi lugha ya Kiswahili kuwa mojawapo inayotumika
kutafsiri filamu na tamthiliya hizi za
michezo
ya kuigiza. Nimesikia mlifanya shindano la vipaji vya sauti ambapo
watanzania kumi walipatikana na watakwenda kufanya kazi katika makao
yenu makuu yaliyopo Beijing.
Hii ni hatua nzuri
na jambo la kuigwa kwa kukipa Kiswahili nafasi kubwa. Ninegependa
kumalizia kwa kutoa wito kwa washindi waliopatikana kwenda huko China
kutuwakilisha vema kama mabalozi wetu na kukifanya Kiswahili kiendelee kutambulika zaidi.” alisema Wambura
Akielezea
umuhimu wa maonyesho hayo Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,.
Guo ZiQi amebainisha kuwa kihistoria China imedumisha kwa dhati urafiki
na mataifa ya Afrika na kushirikisha tamaduni ndio njia madhubuti
itakayoenzi mahusiano hayo.
‘’Utofauti
ndio unaofanya dunia pawe mahala pazuri pa kuishi na China na Tanzania
kwa muda mrefu zimedumisha utamaduni wao unaovutia zaidi. Katika kilele
cha mkutano wa jukwaa la ushirikiano baina ya China na Afrika
uliofanyika mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya watu wa China,
Xi
Jinping alionesha nia ya kujizatiti katika kudumisha mahusiano mazuri
ya kiutamaduni, kuimarish mafunzo baina ya China na Afrika ili kusonga
mbele kwa pamoja na vilevile kuhakikisha mustakabali wa ukuaji wa
urafiki baina ya China na Afrika.’’Alisema ZiQi
‘’Kwa
kuendelea kukua kwa mahusiano ya maingiliano ya kiutamaduni baina ya
watu wa China na Waafrika, michezo ya kuigiza ya runinga na filamu za
Kichina imezidi kujizolea umaarufu na kuwa kichocheo muhimu katika
kujenga mahusiano baina ya pande hizo mbili. Kwa hivi sasa Beijing
inaongoza China katika uzalishaji wa michezo ya kuigiza ya runinga na
filamu.
Mpaka
hivi sasa ina taasisi takribani 3,400 zilizojikita katika uzalishaji wa
filamu na vipindi vya uninga na uendeshaji, vikiwa tayari
vimekwishazalisha zaidi ya mfululizo wa vipindi vya runinga 3,000 na
karibuni filamu 300 kwa mwaka.’’ alisema ZiQi
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Teknolojia na Ufundi ambaye alizungumza kwa
niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Wang Xiabo alisema
kuwa,‘’mnamo mwaka 2014, Halmashauri ya Mamlaka ya Uandishi wa Habari,
Uchapishaji, Redio, Filamu na Runinga ya Beijing ilishirikiana na
StarTimes kuzindua msimu wa Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga
na Filamu za Beijing katika nchi za Kiafrika. Lengo kubwa lilikuwa ni
kuleta simulizi nyingi za Kichina barani Afrika na kukuza uhusiano
katika tasnia za filamu na runinga baina ya pande mbili.’’
‘’Maonyesho
haya yamefanyika kwa mafanikio makubwa kwa miaka ya 2014 na 2015
mfululizo. Filamu maarufu za Kichina na mfululizo wa michezo ya kuigiza
ya runinga ambayo imeingizwa sauti kwa lugha ya Kiingereza, Kifaransa
na lugha nyinginezo tano za Kiafrika zilionyeshwa na StarTimes kwa miaka
hiyo iliyopita,’’ alisema Wang Xiabo kuwa,‘’Katika kipindi hiko
tamthiliya kama zilipata mapokezi makubwa sana kutoka kwa hadhira ya
barani Afrika.
Meneja
Mkuu wa Shirika la Utangazaji waTaifa (TBC), Ayoub Riyoba, ambao ni
washirika wa kampuni ya StarTimes katika urushaji wa matangazo ya
dijitali nchini Tanzania amebainisha umuhimu wa filamu hizo hususani
katika ukuzaji wa tamaduni baina ya nchi hizo mbili.
‘’Tanzania
na China zina historia ndefu ya mahusiano tangu enzi hizo za waasisi wa
mataifa haya. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kisiasa, kiuchumi
na kiutamaduni. Sisi kama chombo cha habari cha taifa tumekuwa mstari
wa mbele katika kuhakikisha kuwa tunasaidia jitihada za
serikali
kukuza na kuutangaza utamaduni wetu hususani lugha ya Kiswahili. Kwa
takribani miaka miwili iliyopita TBC imekuwa ikionyesha tamthiliya za
Kichina zilizoingiziwa sauti kwa lugha ya Kiswahili.
Kwa
kufanya hivyo hivyo tamthiliya hizo zimeonyesha kupokewa vizuri na
kupendwa sana na watanzania kwani wamekuwa wakielewa kinachoonekana.’’
alisema Riyoba
‘’Mbali
na kukuza lugha yetu ya Kiswahili nchini na nje yanchi, hii pia ni
fursa kwa tasnia yetu ya filamu kujifunza kutoka kwa wenzetu ambao
wamepiga hatua zaidi. Tasnia yetu bado ni change na inahitaji mengi ya
kujifunza ili kusonga mbele na kufikia pale walipo wenzetu na kuwa
inazalisha kazi nyingi zaidi za sanaa.
Ningependa
kuchukua fursa hii kuipongeza na kuishukuru serikali ya China kwa
jitihada zao wanazozionyesha katika kukuza filamu na lugha yetu ya
Kiswahili. Na ningependa kuwaahidi kutokana na ushirikiano huu
watazamaji wa TBC wataendelea kupata burudani ya tamthiliya
na
filamu nzuri zaidi ya zilizopita.’’ alisema Meneja Mkuuwa TBC katika
maonyesho hayo Ubalozi wa China nchini Tanzania pia ulikabidhi mfano wa
hati za makubaliano ya kwenda kufanya kazi jijini Beijing kwa washindi
10 waliopatikana katika shindano la vipaji vya sauti lililofanyika
mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Washindi
hao 10 waliopatikana ni; Hilda Malecela(DSM), Safiya Ahmed(ZNZ), Saiq
Kututwa(ZNZ), Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala Abdul(DSM), Rukia
Hamdan(ZNZ), Richard Rusasa (DSM), Happiness Stanslaus - Nyamayao (DSM),
Jamila Hassan(DSM) na Abraham Richard (DSM).
No comments:
Post a Comment