Tuesday, September 6, 2016

KIVUKO CHA MV.MAGOGONI CHAANZA KUTOA HUDUMA ZA USAFIRI

Mkuu wa Jeshi la Majini (Navy, Meja Jenerali Rogastian Laswai (kulia) akitoa maelezo Kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa kwanza kushoto) kuhusu huduma za usafiri wa majini katika Kivuko cha Mv. Magogoni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Majini (Navy) Meja Jenerali Rogastian Laswai kabla ya ufunguzi wa Kivuko cha Mv. Magogoni, jijini Dar es salaam.
Muonekano wa Kivuko cha Mv. Magogoni kikiwa majini mara baada ya ukarabati wake kukamilika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kivuko cha Mv. Magogoni mara baada ya ukarabati wake kukamilika, Jijiji Dar es salaam.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng. Manase Ole Kujan (Kushoto), akitoa maelezo ya moja ya kifaa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) mara baada ya ufunguzi wa Kivuko cha Mv. Magogoni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa nne kushoto)akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng.Manase Ole Kujan mara baada ya ufunguzi wa kivuko cha Mv. Magogoni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Kivuko cha Mv.Magogoni, Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa nne kushoto) akiwa pamoja na watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakivuka kuelekea upande wa Kigamboni kwa kutumia usafiri wa Mv. Magogoni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akishuka kutoka katika kivuko cha Mv. Magogoni.
Wakazi wa Kigamboni wakielekea kupanda kivuko cha Mv. Magogoni mara baada ya kuanza kutoa huduma za usafiri kati ya Magogoni na Kigamboni.

No comments: