Na Mwandishi Maalum,
New York
Shirika lisilo la
Kiserikali la
Speak
Up for Afrika limemtunukia tuzo, Rais Mstaafu Jakaya Mrisho
Kikwete kutokana na uongozi wake wa kisiasa na utetezi wake kwa makundi ya jamii yaliyo katika mazingira magumu
hususani wanawake na watoto.
Utoaji wa Tuzo hiyo ya
uongozi wa kisiasa na utetezi , umekwenda sambamba na hafla ya
miaka mitano ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Speak up Afrika. Hafla hiyo iliyofanyika jana Alhamisi Jijini New
York ilikuwa pia ni
sehemu ya kuhamasisha uchangiaji wa shughuli za
Taasisi hiyo.
Mchango ambao umetambuliwa na
Speak Up Afrika, taasisi ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa Karibu na Rais Mstaafu Kikwete, ni katika maeneo ya upelekaji na usambazaji wa huduma za msingi
za afya hususani afya ya mama na mtoto,
udhibiti wa ugonjwa wa malaria kupitia kampeni ya malaria haikubaliki ,usambazaji wa
vyandarua vyenye viatilifu, kampeni
ya lishe bora, na kampeni ya
chanjo kwa watoto.
Pamoja na kutambua
juhudi za Rais Mstaafu Kikwete katika kuyasemea maeneo hayo, Taasisi hiyo kupitia Mkurugenzi wake Mtendaji Bi. Kate Campana pia imemtambua kama kiongozi ambaye amekuwa mstari wa mbele wa kulisema Bara la Afrika kila mara alipopata fursa
ya kufanya hivyo wakati akiwa
madarakani na hata baada ya kustaafu.
Rais kikwete ameelezwa katika hafla hiyo
iliyowashirikisha wadau wa kada
mbalimbali, kama kiongozi wa kisiasa ambaye amezigusa nyoyo za watu wengi
kujitolea kwaajili ya watu wenye mahitajio ya kupata huduma za msingi za
kijamii ambazo au wameshindwa kuzipata
kutokana na kipato kidogo au haziwafikii kabisa.
Akipokea Tuzo hiyo,
Rais Mstaafu Kikwete , amesema Tuzo hiyo
ni ya watoto wote waafrika ambao
ndio waliomfanya asimame mbele
ya wageni waalik
“ Ni kwa sababu yenu ndio sababu nimetenga muda wangu baada ya kustaafu kusukuma mbele agenda
ya kuboresha maisha yanu. Ninafanya
hivyo kwasababu makuzi yangu yalikuwa kama ya mtoto yeyote yule wa kiafrika, nimeyaishi maisha wanayo ishi. Na kwa hiyo ninaelewa fika hamu na kiu yao ya kuwa na maisha bora na afya njema”. Akasema
Kikwete na kushangiliwa na wageni waalikwa.
Akaongeza kuwa , mafaniko ambayo ameyapata katika juhudi hizo za kufikisha huduma za msingi za kijamii kwa makundi yenye mahitaji yametokana na mambo mawili makubwa moja
ni aina ya uongozi alioutumia kusukuma harakati hizo. Na pili uhamasishaji uliofanyika katika kupiga vita malaria kupitia Speak Up Afrika na
kampeni yao ya malaria haikubaliki.
“ Nisingeweza kuyafanya niliyoyafanya bila uungugwaji mkono na ushirikiano
wa karibu nilioupata na ninaoupata
kutoka taasisi za kimataifa ikiwamo hii
ya Speak Up Afrika. Ndio maana kwa mfano,
tumeweza kupunguza visa vya malaria kwa
theluthi mbilli,
tumefanikisha upatikanaji wa
chanjo kwa asilimia 96 kwa watoto wote na kupunguza vifo vitokanavyo na malaria kwa
nusu.” Akaeleza Kikwete na
kushangiliwa tena.
Akasema, anamini katika ushirikiano na wadau mbalimbali kama akina Ray Chambers kupitia kampeni
ya hakuna tena malaria, Taasisi ya Bili na Melinda Gates na Gavi Vaccination Alliance ambayo anashirikiano nayo kwa karibu katika kampeni ya chanjo kwa wote.
Rais Mstaafu
amewahakikishia watendaji wa Speak Up Afrika kwamba ataendelea kufanya kazi nao kwa karibu kutokana
kile alichosema amejionea mwenye kazi nzuri wanayoifana.
Akawasihi wadau mbalimbali kuichangia taasisi hiyo kwa kile alichosema, inafanya kazi kubwa ya siyo tu kufikisha huduma za kijamii pale
zinapotakiwa lakini pia imekuwa ni
kipaza sauti cha Afrika.
Wengine waliopewa Tuzo kwa kutambua michango yao kwa jamii
ni pamoja na Professa Awa Marie Coll- Seck, Waziri wa
Afya wa Senegal, Bibi Toyin Saraki,
mwanzilishi wa Taasisi ya
Wellbeing Afrika ambayo pia imekuwa ikitoa elimu na misaada kwa wanawake na watoto
pamoja na elimu kwa wakunga na kutambua
kazi nzuri, kubwa na ngumu ya
kuwahudumia wanawake wenzao wanapojifungua.
Na Bwana Kabirou Mbodje ambaye ni
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Wari.
Taasisi ya Speak Up
Afrika imeanzishwa na wanawake na inaongozwa na wanawake. Ni
taasisi ambayo imejijengea uweo na sifa kubwa ndani ya kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake.
No comments:
Post a Comment