Na MatukiodaimaBlog.
SERIKALI ya
mkoa wa Iringa
imepongeza msaada mkubwa uliotolewa na kampuni ya Asas
ya mkoa hapa wa ujenzi wa jengo
la kituo
cha damu salama
cha kisasa na ujenzi wa jengo la
watoto wanaozaliwa njiti katika
Hospitali teule ya mkoa
wa Iringa pamoja miradi itakayogharimu zaidi ya Tsh
milioni 400
Katika taarifa iliyosomwa na mganga mkuu
wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Dr Robert salim wakati wa
hafla ya uwekaji wa jiwe la
msingi katika miradi hiyo leo mbele ya
mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
alisema kuwa awali uongozi wa hospitali hiyo
ulimwandikia barua mfanyabiashara huyo
ili kusaidia msaada wa kontena ambalo lingetumika katika kituo cha benki ya damu salama ila mfanyabiashara huyo alijitolea kujenga jengo
hilo la kisasa na kuongeza msaada
wa jengo la watoto wanaozaliwa njiti .
“Kutokana na agizo la Serikali la
kuanzisha Benki za damu salama katika Mikoa..... Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa
kushirikiana na Mfadhili
Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS iliona ni vyema kujenga jengo la Kituo
Kidogo cha damu salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ili kufikia azma hiyo.
...Hospitali ilimuomba Mfadhili huyo atoe msaada wa “Container” kwa ajili ya
shughuli hiyo, lakini Mfadhili kwa kuona umuhimu wa huduma ya damu salama
katika Mkoa aliomba apewe ramani ili ajenge kituo hicho badala ya
kutumia“Container”.”alisema
Dr
Salim alisema kuwa Hospitali hiyo kabla ya mfanyabiashara huyo
kujitolea ujenzi wa jengo
hilo kituo cha kidogo
cha damu salama ulikuwa
ukitegemea damu kutoka
kituo cha kanda kilichopo
mkoani Mbeya ila
sasa wataweza kukusanya
damu kupitia kituo
hicho.
Alisema kuwa lengo la mradi huu ni Kuboresha upatikanaji
wa huduma za damu salama katika Mkoa wa Iringa kutokana na kuongezeka kwa
mahitaji ya damu salama katika Vituo vya kutolea huduma za afya na kupunguza
vifo vya Uzazi, Watoto wachanga, Watoto na Wahanga wa ajali za barabarani na
kuwa lengo la Mkoa kwa mwezi ni kukusanya chupa 784 na kwa mwaka ni chupa 9,413
(units).
Hata
hivyo alisema mahitaji ya damu
kwa mwezi katika Mkoa ni chupa 700 (unit) na katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
ni chupa 160-200 Units kwa mwezi kuwa tangu kituo kianze kutumika mwezi
Februari,2016 Mkoa umekusanya chupa 2,065 (22%) hadi sasa.
“Tunakushukuru mkuu wa mkoa kwa kukubali mwaliko wetu wa kuwa Mgeni Rasmi katika
hafla hii ya kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na
Mfadhili wetu Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS ya Iringa. Katika
hafla hii fupi tutakuomba uweke jiwe la Msingi katika Mradi wa jengo la Kituo
Kidogo cha Damu Salama na Jengo la Wodi ya Watoto wachanga vyote vikiwa ni
hisani kutoka kwa mfadhili
wetu Salim F Abri “
Alisema
kuwa ujenzi huo unafanywa namkandarasi anayenga mradi huu
ni Buyungu General Enterprise wa Iringa chini ya usimamizi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye
amechangia kuchora ramani za jengo hili na kusimamia mradi mpaka ulipokamilika,
mchango wake kama angelipwa ni Tshs.13,939,200.00.
Na
kuwa utekelezaji wa mradi ulianza kutekelezwa
mwezi Novemba, 2014 na umekamilika mwezi Agosti, 2015. Jengo limeanza kutumika
mwezi Februari, 2016. Pamoja na kujenga jengo hili Mfadhili pia ametoa msaada
wa samani, mafriji makubwa 4 ya kutunzia damu na Computer 1 wenye thamani ya
Tshs.30,000,000.00.
`
Aidha, Hospitali ya Vicenza ya
Nchili Italia ilichangia Tshs. 800,000.00 kwaajili ya kusafisha eneo la ujenzi
na Meneja wa Benki ya Damu Salama ya Kanda Mbeya ametoa msaada wa Vitanda 2 vya
kutolea damu, Mizani (weighing scales) za kupimia uzito chupa za damu na Mzani
1 wa kupimia watu wanaojitolea damu.
Alisema Mpaka umekamilika mradi huu wa
kituo cha damu salama umegharimu jumla ya Tshs.154,880,000.00
bila samani na vifaa tiba kuwa faida
kuwa ya mradi huo uboresha utoaji wa huduma
za damu salama kwa kuwa na eneo kubwa la kufanyia kazi,Kupunguza
malalamiko ya wananchi kwa kukosa damu salama.
Pia Kuzuia
maambukizi ya magonjwa ya VVU/UKIMWI, Hepatitis B na C na Kaswende,Kupunguza
vifo vya uzazi, watoto wachanga, watoto na wahanga wa ajali vinavyotokana
upungufu wa damu au kutokwa na damu nyingi,Kupunguza gharama za kufuata damu
salama umbali mrefu (Damu salama Kanda Mbeya) na kuongeza
kuwa Wanufaika zaidi ni
Watoto, Watoto wachanga, Mama
wajawazito, Wahanga wa ajali za barabarani na jamii kwa ujumla.
Dr Salim alisema kupitia mradi huo wanategemea
Kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya huduma isiyoridhisha ya damu salama
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na Halmashauri na kukomesha tatizo la rushwa.
Kuhusu mradi wa jengo la watoto wanaozaliwa njiti
alisema kuwa Mpaka utakapokamilika mradi huu unatarajiwa kugharimu jumla ya
Tshs.309,210,000.00 bila samani na vifaa tiba ambazo zote fedha za mfadhili huyo kampuni ya Asas.
Akizungumzia
hatua ya familia yake kujitolea
kujenga miradi hiyo mikubwa Asas alisema ni kutokana na changamoto kubwa aliyoiona
baada ya kutembelea Hospitali hiyo na hata mmoja kati ya
wanafamilia wake kupoteza mtoto baada ya kuzaliwa njiti na kukosa chumba kwa ajili ya
kunusuru uhai wake.
Mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza
pamoja na kupongeza kampuni ya Asas kwa kujitolea misaada hiyo bado
aliomba wahisani wengine
kuzidi kujitolea kwa ajili
ya maendeleo na kuwa kama mkoa unatambua mchango mkubwa wa kimaendeleo unaofanywa na kampuni ya Asas pia mfanyabiashara Rajan aliyepata
kujitolea kujenga chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo .
Awali mkuu wa
wilaya ya Iringa akimkaribisha mkuu wa mkoa kuweka mawe ya msingi katika miradi
hiyo alisema misaada
anayoendelea kutoka Asas si tu kwa CCM na serikali yake ila hata kwa
vyama vya upinzani na
wakazi mbali mbali wa mji wa
Iringa hivyo kutaka Halmashauri ya Manispaa
kutunza miradi hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza (kushoto) akimpongeza Salim Asas (kulia) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika miradi mikubwa miwili iliyofadhili kampuni ya Asas ukiwemo mradi wa jengo la kituo cha damu salama Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na jengo la watoto wanaozaliwa njiti yote yaliyofadhiliwa kwa zaidi ya Tsh milioni 400 na kampuni hiyo ya Asas ya mkoa wa Iringa(picha na matukiodaimaBlog ) |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akisaini kitabu cha wageni |
Mkurugenzi wa kampuni ya Asas ya Iringa wa tatu kushoto akiwa katika Hafla hiyo |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa miradi hiyo |
Damu iliyochangiwa |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizindua majengo hayo kwa hotuba |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na mfadhili wa miradi ya jengo la Benki ya damu na jengo la watoto njiti wakiweka jiwe la msingi leo anayeshuhudia ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela |
Mkuu wa mkoa wa Iringa akiwa ndani ya jengo la benki ya damu |
Viongozi mbali mbali wakiwa na mkuu wa mkoa kukagua kituo hicho |
No comments:
Post a Comment