Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akiwa ameambatana pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita, jana wakati alipotembea ofisi za Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mst) Ezekiel E. Kyunga (watatu kutoka kushoto), IGP Mangu yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi.
Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mst) Ezekiel E. Kyunga, akitoa neno la ukaribisho kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, ambaye yupo katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi, anayefuata ni kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, SACP Mponjoli Mwabulambo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akifuatilia jambo kwa makini kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mst) Ezekiel E. Kyunga, pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo jana akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akitoa neno mbele ya kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Geita, jana wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chato mkoani Geita, kwa ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi mkoani humo, katikati ni Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe, akifuatiwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, SACP Mponjoli Mwabulambo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, pamoja na timu ya maofisa na kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, SACP Mponjoli Mwabulambo, wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe, alipomtembelea ofisini kwake jana wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, akiwa katika kituo kikuu cha Polisi wilaya ya Chato mkoani Geita, jana alipotembelea kituo hicho wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kipolisi. (Picha zote na Demetrius Njimbwi - Jeshi la Polisi)
No comments:
Post a Comment