Friday, September 16, 2016

Airtel yazindua Kampeni kabambe ijulikanayo kama “Sibanduki”

 Mkurugenzi wa mawasilianoa wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya (kulia)  pamoja na Mkurugenzi wa masoko wa Airtel, Isack Nchunda kwa pamoja wakionyesha bango la kampeni mpya  ijulikananayo kama “Sibanduki... mamba yote yako huku” inayotoa ofa kabambe kwa wateja wapya na faida zaidi kwa wateja wake kwenye  huduma na bidhaa zake. Sibanduki kampeni inatoa  ofa kambambe ya dakika 60 sms 200 na MB bure kwa wateja wapya.
---------------------------------------
Katika kuendelea kutimiza ahadi na dhamira yake ya kutoa huduma za kibunifu na za kipekee kwa wateja wake , Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua kampeni yake mpya ijulikanayo kama “Sibanduki” kwa wateja wake nchi nzima. 
Kampeni ya “Airtel Sibanduki” inaainisha dhamira ya Airtel kuwawezesha watanzania kufungua njia na kuzifikia ndoto zao  pamoja na  kufurahia bidhaa na huduma mbalimbali za kibunifu zilizotengenezwa mahususi katika kutatua changamoto na mahitaji yao kama vile vifurushi vya yatosha, huduma ya Airtel Money Timiza, Kutuma pesa bure, Huduma za kibenki na nyingine nyingi. 
Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa masoko wa Airtel, Isack Nchunda alisema “Tunajisikia fahari kutoa bidhaa na huduma za kipekee zinazokidhi mahitaji  ya muhimu kwa wateja wetu. “Airtel Sibanduki” kampeni yenye kauli mbiu ya “ Mambo yote yako huku” inatoa uhakika na kukidhi mahitaji ya wateja wetu  katika huduma na bidhaa tunazotoa  hivyo kuwapa sababu ya kuendelea kutumia bidhaa na huduma zetu” 
“Airtel Sibanduki” imelenga kwenye huduma muhimu na za kipekee zinazomuwezesha mteja kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii kama vile huduma ya Vifurushi vya Yatosha inayompa Zaidi Mteja kuliko mtandao mwingine Dakika, MB na SMS. Huduma ya Timiza  inayotoa mikopo ya haraka na salama kwa wateja na mawakala wa Airtel Money wakati wowote mahali popote kupitia simu zao za mkononi.  Kupitia huduma hii wateja wanauhakika wakupata mikopo inayowasaidia kuboresha biashara zao na kutatua changamoto mbalimbali” alisema Nchunda 
Aliongeza kwa kusema,  “Airtel Money “Okoa Mapene”  inawawezesha wateja wa Airtel Money kutuma na kupokea pesa bure na kutuma kwenye mitandao mingine kwa unafuu na uhakika zaidi, vilevile mteja wa Airtel money anaweza kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti yake ya benki kwenda kwenye akaunti zao za  Airtel Money wakati wotote. Kwa kupitia mawakala zaidi ya 50,000 walioenea nchi nzima na walioko katika maeneo ambayo hakuna huduma za kifedha za mitandao mingine  simu za mkononi  tunawawezesha wateja wetu kuweka na kutoa pesa kwa urahisi na usalama. 
Sambamba na Airtel Money, Vifurushi vya Airtel yatosha zinatoa uhuru kwa wateja kujitengenezea vifurushi vya muda wa maongezi , ujumbe mfupi na vifurushi vya data. kupitia huduma ya Airtel yatosha tunawawezesha wateja kupata vifurushi vinavyowapa dakika,MB na SMS zaidi . Lengo letu ni kuhakikisha huduma za mawasiliano zinaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi kwa vile huduma za simu si anasa bali ni moja ya mahitaji muhimu
Nchunda aliongeza kwa kuwahasa watanzania wajiunge na familia ya Airtel kwa kutumia bidhaa na huduma ili kufurahia ofa kabambe inayopatikana kama vile ya  kujitengenezea vifurushi wanavyovipenda na pia kupata muda wa maongezi wa dakika 60, SMS 2000 intaneti ya MB 200. Ofa hii ni kwa mteja yoyote atakayejiunga na huduma zetu sasa nchini nzima. Kuwa sehemu ya mtandao wa smaphote na endelea kufurahia ofa na huduma za Airtel. “Sibanduki” kampeni inalenga kuwapa wateja sababu zaidi za kujiunga na kuendelea kutumia Airtel

No comments: