Thursday, August 18, 2016

WIZARA YA FEDHA YAOMBWA KUONGEZA BAJETI YA HUDUMA ZA UZAZI WA DHARURA- ROSE.

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WIZARA ya Fedha yaombwa kuongeza Bajeti ya huduma za uzazi za Dharura hadi kufikia asilimia 100 ili kuokoa maisha ya kinamama na watoto wa changa wakati wa kujifungua.

Ameyasema hayo Mratibu wa Kitaifa wa White Ribbon Alliance, Rose Mlay  wakati akitoa mafuzo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa Serikali iweke wigo wa fedha zinazopangwa kwaajili ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi isitumike kwa shughuli nyingine.

Rose amesema kuwa Vifo vitokanavyo na uzazi havivumiliki, wilaya zote za kila mkoa ziweke kipengere cha huduma kamili za uzazi za zarura(CEmoNC) ili kuondokana na vifo vya mama na mtoto wakati wakujifungua.

Amesema kuwa vifo vingi vya akina mama na watoto vinatokana na mambo mbalimbali hasa ukosefu wa huduma kamili za Uzazi za Zarura  katika hospitali, upungufu wa Damu salama na kuwa na wakunga wasio na ujuzi katika hospitali.
 Mratibu wa Kitaifa wa White Ribbon Alliance, Rose Mlay akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutoa mafunzo juu ya kutokomeza Vifo akinamama na watoto wachanga vitokanavyo na uzazi.

Mtoa Maada na Mshauri wa Maswala ya Habari, Chiku Lweno akitoa maada kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 Meneja Mtetezi wa Mradi wa The White Ribbon Allince, Sizarina Hamisi akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mafunzo hayo yaliyotolewa na wafanyakazi wa White Eibbon Allince jijini Dar es Salaam leo.

No comments: