Friday, August 19, 2016

WANAWAKE WIZARA YA MAMBO YA NJE WAMUAGA BALOZI MULAMULA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba akiongea na Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje walioshiriki katika kikao cha kumuaga Balozi Liberata Mulamula, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Balozi Mulamula ambaye amestaafu utumishi wa umma alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke kuongoza Wizara ya Mambo ya Nje pia mlezi wa Umoja wa Wanawake wa Wizara hiyo (Nje Women). Mhe. Naibu Waziri alimshukuru Balozi Mulamula kwa kuimarisha umoja wa wanawake wa Wizara na kuahidi kuendelea kuenzi mchango wake kwenye umoja huo.
Balozi Liberata Mulamula akitoa neno la shukrani kwa Wajumbe (hawapo pichani) ambapo aliwaasa kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa bidii huku wakizingatia weledi ili kuwa mfano bora kazini, kwenye familia na taifa kwa ujumla.
Balozi Mulamula akimkabidhi Naibu Waziri, Mhe. Kolimba mwongozo wa Umoja huo baada ya kuchaguliwa kuwa Mlezi mpya.
Sehemu ya Watumishi wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia kikao.
Sehemu nyingine ya Watumishi hao wakifuatilia kikao
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake, Bibi. Amisa Mwakawago akitoa taarifa fupi ya Umoja kwa mama mlezi mteule na kwa Wajumbe wengine walioshiriki kikao. Kulia ni Katibu wake, Bi. AnnaGrace Rwalanda.
Dkt. Kolimba akimkabidhi zawadi Balozi Mulamula.
Bibi. Mwakawago akimkabidhi Balozi Mulamula zawadi ya picha yake ya kuchorwa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawsiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni mjumbe wa Umoja wa Wanawake (Nje Women) akitoa neno la shukrani kwa Balozi Mulamula.
Kikao kikiendelea
Picha ya Pamoja ya walezi na uongozi wa Nje Women
Picha ya pamoja.

No comments: