Wednesday, August 3, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja iliyopo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto. https://youtu.be/7qjgq5wrzaI

SIMU.TV: Baraza la taifa la elimu ya ufundi stadi NACTE limevifutia usajili vyuo vitano na kuvizuia kuendelea kutoa elimu ya ufundi stadi. https://youtu.be/V5s4LbszEPg

SIMU.TV: Maafisa kutoka kituo cha haki za binadamu LHRC wametembelea kampuni ya Africa Media Group ili kuendeleza ushirikiano wao wa kutoa elimu kuhusu haki za binadamu. https://youtu.be/72cgMXhwXxk

SIMU.TV: Waziri  mkuu Kassimu Majaliwa amekataa kupokea madawati ya msaada yaliotolewa na wakala wa misitu nchini TFS kutokana na kutengenezwa chini ya kiwango.https://youtu.be/sYSz3jo4TZw

SIMU.TV: Watu wawili wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa kosa la matumizi mabaya ya mtandao. https://youtu.be/knR4lyGJMc4

SIMU.TV: Wafanyakazi wa kampuni ya usafirishaji jijini Dar es Salaam UDART wamegoma wakishinikiza uongozi wa kampuni hiyo kuwalipa mishahara yao ya miezi miwili.https://youtu.be/_IL-Ia12Ph8

SIMU.TV: Alex Kweka mkazi wa Shirimatunda mjini Moshi anaomba msaada wa kupata shilingi milioni 20 ili aweze kwenda kufanyiwa matibabu ya mgongo nchini India.https://youtu.be/wwjJaKLi2WI

SIMU.TV: Serikali ipo mbioni kutafuta mwekezaji atakayewekeza katika kiwanda cha chai kilichopo wilayani Kilolo mkaoni Iringa kilichosimama kwa zaidi ya miaka ishirini sasa.https://youtu.be/szAwMoKyDGg

SIMU.TV: Waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo amekutana na wachimbaji wa makaa ya mawe ili kujadili namna ya kuboresha uchimbaji wa madini hayo.https://youtu.be/YlKUUEk-EKc

SIMU.TV: Treni ya kwanza iliyobeba zao la pamba ikitokea mikoa ya kanda ya ziwa imewasili jijini Dar es Salaam baada ya kusimama kwa usafirishaji kwa njia ya reli kwa muda mrefu.

SIMU.TV: Timu za majeshi za JWTZ zimekabidhiwa bendera ya taifa kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano ya majeshi huko nchini Rwanda. https://youtu.be/n_ByNs275E0

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Mwanza amekuwa wa kwanza kujisajili kushiriki katika mashindano ya mbio maarufu kama rock city marathon. https://youtu.be/oif-J5u0fRc

SIMU.TV: Tamasha la mazoezi ya viungo na mbio fupi za kilometa tano linatarajiwa kufanyika August 6 katika viwanja vya Leaders jijinI Dar es Salaam.https://youtu.be/kkl3CpP7pDo

SIMU.TV: Mikoa mbalimbali inatarajiwa kushiriki katika mashindano ya Pool table ya nane nane ambapo mpaka sasa mikoa kadhaa imethibitisha kushiriki.https://youtu.be/OiMF3PwhiGs

No comments: